JAMII YAHIMIZWA KUONGEZA USHIRIKIANO ILI KUMALIZA UDHALILISHAJI UDHALILISHAJI
NA FATMA HAMAD FAKI PEMBA 23/11/2022.
Jamii
imetakiwa kuacha tabia ya kuzifanyia
suluhu mitaani kesi za udhalilishaji wa kijinsia na badalayake
wasimame mahakamani kutoa
ushahidi ili kupunguza ukatili kwa
wanawake na watoto.
Ushauri huo
ametolewa na mwenyekiti wa kamati za asasi za kiraia Nassor Bilal Khamis wakati
akitoa tarifa kwa vyombo vya habari katika kuelekea shamra shamra ya madhimisho ya siku 16 za
kupinga ukatili kwa wanawake na watoto huko tamwa chake chake Pemba.
Amesema bado matendo ya udhalilishaji yafanyika kila
siku katika shehia zetu, hivyo ni wakati jamii kuondosha rushwa muhali ili
kuona wahanga wa matukio hayo wanapata haki zao stahiki.
‘’kwa kweli
jamii imekua na muhali mkubwa juu ya kusimama mahakamani na kutoa ushahidi kwenye
vyombo vya kisheria matukio ya udhalilishaji’’ alisema mwenyekiti.
Amesema kwa
mujibu wa ripoti za takwimu za ukatili na udhalilishaji wa kijinsia Zanzibar takwimu kutoka ofisi ya mtakwimu
mkuu wa Serikali jumla matukio 131 ya
ukatili na udhalilishaji yameripotiwa katika kipindi cha mwezi Agosti 2022 mwaka huu ambapo wanawake ni 12, Watoto 119
miongoni mwao wasichana ni 84 na
wavulana 35.
Kwa upande
wake mratibu wa chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania Zanziba [Tamwa] ofisi
ya Pemba Fathiya Mussa Said amewasihi wanasheria wanaosimamia kesi mahakamani kufuata madili na miko ya kazi
zao.
‘’Niwaombe
mawakili msimamie kesi kwa mujibu wa
madili yanu kwani leo kafanyiwa mtoto wa mwenzako kesho atafanyiwa wa kwako’’
alisema mratibu tamwa.
Madhimisho
ya 16 za kupinga ukatili na udhalilishaji yatanza rasmi tarehe 25 mwezi huu
ambapo kutakua na shughuli mbali mbali ikiwemo utolewaji wa elimu ya
udhalilishaji na jinsi ya kuripoti katika vyombo vya sheria kupitia shehia na
kwenye madrasa kwa wilaya zote za pemba.
Comments
Post a Comment