MAKOSA 25 WIZI WA KARAFUU YARIPOTIWA POLISI KUSINI PEMBA MSIMU HUU.

 


Jumla ya matukio 25 ya wizi wa karafuu yameripotiwa katika Jeshi la  Polisi Mkoa wa Kusini Pemba tokea kuanza kwa msimu wa  mavuno ya karafuu mwaka huu.

Akizungumza na wandishi wa habari huko ofisini kwake kamanda wa Polisi Mkoa  huo  Richad Tadei Mchovu amesema matukio hayo yalioripotiwa ni wizi wa karafuu mbichi.

Aidha amesema katika matukio hayo pia wamefanikiwa kuwashikilia vijana 27 wanaojihusisha na uhalifu wa karafuu.

Aidha amesema katika matukio hayo  makosa 12 tayari yamepelekwa  Mahakamani ambapo kijana mmoja ameshafungwa jela.

Sambamba na hayo amewataka wananchi Kisiwani Pemba kuendelea na uchumaji wa zao la karafuu kwa Amani  bila kufanyiana vitendo vyovyote vya kihalifu.

Amewataka wananchi kuuza karafuu  zao katika Shirika la ZSTC, ili wawezekuisadia Serikali mapato.

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.