WIZARA HABARI YATAKIWA KUINGIZA TIMU ZHA NETBAL KATIKA MASHINDANO YA MAWIZARA

 

 

SALIM HAMAD,PEMBA

MDAU wa Michezo Kisiwani Pemba Raya Mkoko Hassan ,Ameishauri Wizara ya Habari Vijana Sanaa na Michezo ambayo inaanda michuano ya mawizara  kuingiza  timu za Netbal katika mashindano ya Mawizara ili kuona  akina mama nao  wanapata nafasi za kuonesha Vipaji vyao.

 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema Wizara ya habari inapaswa kuangalia suala hilo kwani nao akina mama  wana uwezo mkubwa wa kupambana kwenye mashindano kama hayo.

Alisema kuwepo kwa mashindano hayo kwa upande wa Netbali itakuwa ni jambo zuri ambalo  litasadia kukuza uhusiano na Afya zao kutokana na kuwa michezo ni afya.

 ‘’Tunaishauri Wizara husika iliyoandaa mashindano ya Mawizara kuangalia uwezekano wa kuingiza timu za Netbal ambazo zitaweza kuonesha uwezo na Vipaji  kwa akina mama ‘’alisema.

Alisema kafuatia mashindano hayo yamewapa hamasa wanawake nao kuona wanakuwemo kwenye mashindano hayo kwa kila wizara kuwepo kwa timu moja ya wanawake ili waweze kufika mbali.

 Hata hivyo amewataka wadau na Wapenzi kuhakikisha wanaunga mkono maswala ya michezo  kwani yamekuwa yaki chochea umoja na uhusiano mwema miongoni mwa watumishi.


 

 

 

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.