WANDISHI WATAKIWA KURIPOTI MATATIZO YAO MCT WAKATI YANAPOWATOKEZEA
WAANDISHI
wa habari nchini, wametakiwa kushirikiana na Baraza la Habari Tanzania [MCT]
kutoa malalamiko yao wakati wanapopata matatizo katika majukumu yao ya kazi.
Hayo yamesemwa na Afisa ufuatiliaji na tathmini wa MCT Paul Mallimbo wakati akizungumza na wandishi wa habari huko
Zanzibar, ambapo amesema Baraza kwa kuwajali wandishi wa habari, limeweka
utaratibu wa kupokea kero zinazowakumba ikiwemo kupigwa, kutukanwa, kunyimwa
taarifa ili kuweza kutoa msaada kwao.
Amesema imeonekana bado wandishi hawajakuwa na mwamko wa
kuripoti matatizo yao, wakati yanapowatokezea na jambo ambalo linawanyima fursa
yao ya kufanya kazi zao kwa umakini.
Kwa upande mwengine ameitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
kutoa mashirikiano ya hali ya juu wandishi wa habari, jambo ambalo itawafanya
waweze kuandika na kuripoti habari zenye ukweli na zenye kuleta mabadiliko
mazuri katika Jamii.
Mapema Mtendaji wa Baraza la habari Tanzania [ MCT] ofisi ya
Zanzibar Shifaa Said Hassan, amewasihi wandishi wa habari kushirikiana kwa
pamoja katika majukumu yao ya kazi, jambo ambalo litawawezesha kufanya kazi zao
kwa uwadilifu wa hali ya juu.
Nao baadhi ya wandishi waliohudhuria mkutano huo wamesema,
wapo baadhi ya wandishi wanakumbana na vikwazo tofauti katika kazi zao, lakini
bado wanakaa kimya jambo ambalo linawafanya waendelee kunyanyasika siku hadi
siku.
Comments
Post a Comment