WANDISHI WA HABARI WAHAMASISHENI WANAUME KUPIMA VVU
Hayo
yamesemwa na mkurugenzi wa tume ya ukimwi Zanzibar [ZAC] Ahmed Mohd wakati akizungumza na
wandishi wa habari huko Gombani chake, amesema wandishi wana mchango mkubwa juu
ya kuwaelimisha wanaume kupima afya zao jambo ambalo litaepusha ongezeko la
mambukizi mapya ya virusi vya ukimwi Nchini.
Amesema
imebainika kuwa idadi ya wanaume wanaojitokeza vituoni mwa afya kupima VVU ni ndogo
ukilinganisha na wanawake.
‘’Wanaume
bado hawataki kupima afya zao, wengi ni wanawake ndio wanaozitumia huduma
hizo,’’Amesema dk Ahmed.
Amesema wanaume wengi wanaogopa kupima vvu kutokana
na kutokuwepo kwa usiri kwa baadhi ya madaktari wanaotoa huduma hizo,
jambo ambalo linachangia kwa kiasi
kikubwa kuongezeka kwa mambukizi mapya ya virusi vya ukimwi.
Amesema
wanaume wengi kipimo chao kikubwa ni wake zao, kwani wanahisi wakishakwenda
kupima na kuonekana wako salama na wao hujihisi hawana mambukizi.
Ameeleza
kuwa tokea kugundulika ugnjwa huo hapa
Visiwani mnamo mwaka 1986 wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani wameweza
kudhibiti mambukizi hadi kufikia 0.4
Akitaja
idadi ya watu wanaoishi na vvu hapa Zanzibar ni 7020 ambapo wanawake ni 4828,
wanaume ni 2,192, wanaotumia dawa kwa upande wa wanawake 4774 na wanaume ni
2168.
Mapema kaimu
mratibu wa tume ya ukimwi ofisi ya Pemba
Ali mbarouk Omar amesema wandishi wa
habari wana nafasi kubwa katika kuwashajiisha wanaume kushiriki katika huduma
za afya.
Nae mkufunzi
wa mafunzo hayo Abuu bakar Ibrahim Msemo amesema wakati umefika kwa wandishi wa
habari kuandika zenye kuonyesha tabia hatarishi ili wanaume waweze kuzifahamu
na kujiepusha nazo.
Comments
Post a Comment