WAZAZI WAHIMIZWA KUWAPATIA ELIMU WATOTO WENYE ULEMAVU
Wazazi na walezi wenye watoto walemavu wametakiwa kuwapeleka mashuleni pamoja na madras ili waweze kupata elimu ambayo itawafaa katika maisha yao ya badae.
Ushauri
huo umetolewa na mmoja wa mzazi wa mtoto wenye ulemavu wa viungo hapa kisiwani Pemba amesema watoto wenye
ulemavu nawao wana haki ya kupata elimu kama watoto wengine.
Amesema
wapo wazazi wamekua wakiwafungia ndani, watoto wao wenye ulemavu, jambo ambalo
limekua likiwakosesha fursa mbali mbali ikiwemo elimu.
‘’Nawaomba
wazazi wenzangu msiwafungie ndani watoto walemavu, kwani mkiwaeka ndani watakua
wanadumaa na mnawatia maradhi, Alisema mama mwenye mtoto mlemavu.
Amefihamisha
kuwa watoto walemavu maranyingi hufanya vizuri katika masomo yao ukilinganisha na
wengine wasio na ulemavu.
Akitoa
ushuhuda amesema wakati mtoto wake
mlemavu hajapata kigari cha kuendea shule alikua hachangamki na alikua
akiwaona wenzake wanakwenda shule akijitia chumbani na kulia.
Hivyo
kwa sasa amefanikiwa kupata kigari, anakwenda shule na anachangamka na wenzake,
tofauti na pale alipokua haendi shule.
Kwa
upabnde wake Afisa wa elimu
mjumuisho Ali Khamis Kombo amesema wizara imeanzisha elimu
mjumuisho katika shule za mjini na Vijijini ili kuona watoto wenye ulemavu na
wao wanapata haki yao ya elimu.
Nae
mratibu wa idara ya watu wenye ulemavu ofisi ya Pemba Mashavu Juman
Mabrouk amesema wameweka mikakati
madhubuti wa kutoa elimu kwa jamii ili
kuona watoto waenye ulemavu wanapata haki zao za msingi ikiwemo Elimu, Afya.
Comments
Post a Comment