KIJANA OMAR ALI HAJI ATUPWA RUMANDE KWA KUTISHIA AMANI.


 

Mahakama ya Mkoa C Chake chake imemsokomeza rumande  kijana Omar Ali Haji  mwenye umri wa miaka 18  mkaazi wa junda miti kiwani  akidaiwa  kutishia amani,  baada ya kushindwa kutimiza masharti ya zamana aliyopewa na mahakama hiyo.

Hakimu wa mahakama hiyo Rashid  M Magendo  amesema kijana huyo ataendlea  kusota rumande  hadi tarehe 30/ mwezi huu kwa ajili ya kusikilizwa,  huku akiwa na wadhamini  wake wawili [2] na shilling laki tatu [30000], kwa ajili ya kupewa dhamana yake.

Mtuhumiwa  huyo wakati yupo  kizimbani na kusubiri asomewe shitaka lake mwendesha mashtaka  wa Serikali kutoka ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka DPP Mohd  Said Mohd amesema sena pingamizi nimekubaliana na uawamuzi huo.

Imedaiwa kuwa siku ya tarehe 23/ 7/ mwaka huu majira ya sa moja  na nusu asubuhi  huko Junda miti  Kiwani wilaya ya Mkoani Pemba ulimshambulia kwa hatari Khamis Juma Ali kwa kumkata na Panga katika sehemu zake za mkononi na kusababisha kupata maumivu makali katika sehemu hizo jambo ambalo ni kosa kisheria kifungu cha 204 [a] sheria nambari 6/ 2018 sheria ya Zanzibar.

 

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.