TASISI ZA KIHABARI ZATAKIWA KUWEKA SERA ZA UDHALILISHAJI
NA FATMA
HAMAD FAKI.
Mwenyekiti
wa chama cha wandishi wa habari wanawake Tanzania [TAMWA] Joic Shebe amesema kuweko na mfumo maalum ambao
utawasaidia wandishi wa habari kuripoti malalamiko yao wakati wanapofanyiwa
unyanyasaji wa kingono katika tasisi zao.
Mwenye kiti
huyo ameyasemahayo katika mdahalo kuhusu unyanyasaji wa kingono katika tathnia
ya habar kwa wandishi wa habari
uliofanyika kwa njia ya mtandao amesema bado wandishi wa habari wanawake
wanakumbana na unyanyasaji wa kingono wakati wanapokua katika harakati zao za kazi.
Amesema kwa
mujibu wa utafiti uliofanywa unaonesha kuwa kila penye watu wawili mmoja amefanyiwa
unyanyasaji, hivyi ni vyema kwa vyombo vya habari vitunge sera na kuhakikisha zinafuatwa kwa mujibu wa sheria
ili kutoa adhabu kali kwa wale watakao jihusisha na vitendo hivyo.
Akiwasilisha
mada ya sera ya jinsia katika vyombo vya habari Nevil Meena amesema wandishi wa habari ndio mwanga kwa
jamii, hivyo wasikubali kufanyiwa unyanyasaji wa ngono kwa ajili tu ya
kujipatia maslah.
Mapema
Afisa program wa Baraza la habari
Tanzania [ MCT] Zanzibar Shifaa Said Hassan amesema kwa mujibu wa utafiti ulioufanywa
umeonyesha kuwa vyombo vingi vya habari havina sera ya unyanyasaji, hivyo ipo
haja kuwepo na ufuatiliaji wa hali ya juu ili kupata tarifa sahihi za unyanyasaji
kwa wandishi wa habar.
Naibu waziri
wa habari Tanzania Paulina Gekul amesema
kila mzazi anatamani mtoto wake atimize ndoto zake bila vikwazo vyovyote ,hivyo
basi ni budi kila mmoja kwa nafasi yake alionayo awe mlinzi na mlezi kwa mtoto
wa menzake.
Aidha
amewasihi wandishi wa habari wanawake wajiheshimu, kujilinda na kufuata maadili
yao kwani kufanya hivyo kutawaepusha na udhalilishaji.
Nae priska Ishamba
mwandishi na mtangazaji wa wa Cloud tv amewashauri wandishi wenzake wasivunjike
moyo wakati watakapo pata vikwazo kama
hivyo bali watoe tarifa na waendelee kuchapa kazi ili hali tu wafuate sheria na
madili yao.
Mdahalo huo
kuhusu udhalilishaji katika tasisi za habari kwa wandishi wa habari umeandaliwa
na Jukwa la wahariri Tanzania kwa kushirikiana na shirika la Internws Tanzania.
Comments
Post a Comment