WANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUWAPA ELIMU JAMII JUU YA USULUHISHAJI WA MIGOGORO
Wandishi wa
habari wametakiwa kuwaelimisha jamii kwa kuandika habari za utatuzi wa migogoro
kama ya Siasa, Ndoa ili waweze kujiepusha na migogoro isiyo ya lazima.
Akizungumza
katika mkutano juu ya namna ya utatuzi wa migogoro katika Jamii Afisa
ufuatiliaji na tathmini kutoka kituo cha huduma za sheria Zanzibar Khamis
Haroun Hamad huko gombani Chake chake Pemba.
Amesema wandishi wana nafasi kubwa katika jamii hivyo
ni wajibu kutumia kalamu zao kwa kuielimisha jamii kujiepusha na migogoro isiyo
ya lazima jambo ambalo litapelekea kuvunjika kwa Amani.
Amesema
suala la kulinda amani si la mtu peke yake bali kila mmoja kwa nafasi yake
anapaswa achukue tahadhari juu ya kulinda haki za mwenzake.
Mapema
mratibu wa mradi wa Jenga amani yetu
kutoka kituo cha huduma za sheria Zanzibar Jamila Masoud amesema wakati
umefika kwa wandishi wa habari kujikita zaid Vijijini katika kazi zao jambo
ambalo litawasaidia kuibua migogoro ambayo inajitokeza na kuweza kuzitolea
suluhu.
Nao baadhi
ya washiriki wa mkutano huo wamesema imeonekana migogoro ya Ardhi pamoja na
kindoa ndio inayojitokeza zaid katika Jamiim, hivyo ipo haja kuwepo na mashiriano ya pamoja kati
ya wadau na viongozi wa mradi huu kuelekeza nguvu zao zaid katika maeneo hayo ili kuona jamii inaondokana na hilo.
Mafunzo hayo
yaliojumuisha wadau mbali mbali wakiwemo wandishi wa habar, mahakama ya Ardhi, Dawati
la jinsia, Masheha ambapo lengo la mradi
huo ni kuona jamii inadumisha amani yameandaliwa na shirika la Seach fer Common
Ground kwa kushirikiana na Kituo cha huduma za Sheria Zanzibar, Kituo cha
sheria na haki za binadamu kwa ufadhil wa Umoja wa ulaya.
Comments
Post a Comment