AFUNGWA KWA KUBAKA
Kushindwa
kudhibiti matamanio yake kumempelekea
Kijana Thani Khamis Mohd 22 mkaazi wa Kinyasini Mkoani Pemba kutumikia
Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miaka 14, pamoja na fidia ya shiling milioni mbili
(2,000,000)/.
Hakimu wa
mahakama ya mkoa A Chake chake Abdul Razak Abdul kadir amesema hukumu hiyo
imekuja baada ya mahakama yake kujiridhisha kutokana na ushahidi uliotolewa na
mashahidi.
Hivyo
mahakama imeamua kumtia hatiani mtuhumiwa huyo, na endapo atashindwa kulipa
fidia atatumikia tena kifungo cha miezi 6.
‘’Mahakama
yangu imeridhika na ushahidi uliotolewa ndipo ikatoa hukumu na endapo
atashindwa kulipa fidiya atatumikia tena kifungo cha miezi 6,’’ alisema hakimu.
Mwendesha mashtaka wa Serikali kutoka ofisi ya
mkurugenzi wa mashtaka Seif Mohamed Khamis amekubaliana na hukumu hiyo, kwani
itakua ni fundisho kwa wabakaji.
Aidha
amewataka wananchi kushirikiana na mahakama kutoa ushahidi ili kuona kesi za udhalilishaji zinapata
hatia jambo ambalo litapunguza vitendo hivyo katika Jamii.
Awali iIielezwa
mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo siku
ya terehe 21 /7/ 2018 majira ya saa 7:00 mchana huko eneo la Mkirikiti Kinyasini
wilaya ya Mkoani, Pemba alijaribu kutaka
kumbaka msichana wa miaka 12.
Kufanya
hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 111[1] [2], [a] cha sheria nambari 6 ya
2018, sheria ya Zanzibar.
Comments
Post a Comment