WIZARA YA AFYA YAHIDI KUBEBA UBINGWA YA WIZARA CUP

SALIM HAMAD,PEMBA

 BAADA ya kufanikiwa kutinga katika fainali ya Michuano ya Mawizara (Wizara Cup)  Nahodha wa timu ya Wizara ya Afya Abdul Karim Abdi Heri ameapa kuwa watabeba ubingwa katika michuano hiyo.

 Akizungumza na Mwanaspoti mara baada ya kufanikiwa kutinga kwenye hatua hiyo kwa kuichapa timu ya Shirika la Umeme ‘’Zeco’’  mabao 2-0 katika mchezo wa Nusu Fainali  uliopigwa Uwanja wa Gombani, Nahodha huyo alisema ushindi huo umewapa asilimia kubwa ya kufanya  vizuri kwenye Fainali ya mashindano hayo.

 Alisema haikuwa kazi rahisi kuweza kuwafunga wapinzani wao kutokana na wao kutafuta nafasi ya kuwania kucheza fainali ya Mashindano hayo ili waweze kubeba ubigwa kwamara ya kwanza tokea kuanzishwa kwa mashindano hayo.

 Alisema katika mchezo huo  walipambana na kuonesha umahiri mkubwa kwa kushinda mchezo huo uliokuwa mgumu kwenye hatua hiyo iliyo kuwa inawaniwa na wapinzani wao.

‘’Sisi tumejipanga sana katika mashindano hayo licha kuwa ni magumu lakini tunaahidi washabiki wetu kwamba tutabeba taji la mashindano hayo kwa mara ya kwanza’’alisema .

 Hata hivyo alisema kutokana na uwezo mkubwa walionesha  kwenye mchezo huo anaamini  kwa kiasi kikubwa  wateweza kufanya Vyema ili kutwaa kombe la michuano hiyo.

 Akizungumzia muendelelezo wa Michuano hiyo Msemaji wa timu hiyo Hassan Said alisema michuano hiyo imekuwa na msisimko kama michuano ya ligi daraja la kwanza taifa iliyomalizika hivi karibuni.


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.