UHABA WA WALIMU MJUMUISHO NI CHANGAMOTO KUBWA KWA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU MASKULINI
Wazara elimu na mafunzo ya amali Zanzibar imetakiwa kuwafundisha walimu wengi elimu mjumuisho ili wawe na uwezo wa kuwasomesha wanafunzi wenye ulemavu maskulini.
Hayo
yamesemwa na mama wa Mtoto mwenye ulemavu wa viungo Siwawi Omar Said wakati
akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko nyumbani kwake Kijichame wilaya ya Micheweni Pemba, amesema walimu
wengi wanaofundisha maskulini hawana taaluma ya kufundishia wanafunzi wenye
ulemavu.
Amesema
watoto wenye ulemavu wamekuwa wakipata shida, kwani hawaelewi wanachofundishwa,
hivyo ni vyema wizara ya elimu kuwafundisha walimu lugha mbali mbali kulingana
na mahitaji ya mlemavu mwenyewe.
‘’Ni vyema
kuwepo na walimu wenye taluma ya kufndisha walemavu, kwani bila kufanyiwa hivyo
wanakua hawaelewi lolote watakua wanakwenda wakicheza tu huko maskulini,’’
Alisema mama.
‘’Nivyema somo la watu wenye ulemavu likaingizwa kwenye
mtaala wa elimu, kwani kutawafanya walemavu waweze kufahamu vizuri masomo yao
wanapo fundishwa’’, wameeleza Wadau.
Kwa upande
wake Afisa Mdhamini Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar wa Kisiwani Pemba Ahmed Abuubakar amesema
mtaala uliopo sasa ni changamoto
kubwa kwa elimu mjumuisho.
Nae Afisa
elimu mjumuisho pemba Ali Khamis Kombo amekiri kuepo kwa changamoto ya upungufu
wa walimu wa elimu mjumuisho maskulini.
Hivyo
amewataka wazazi kuwa na subra kwani wizara iko kwenye mchakato wa kuhakikisha
elimu mjumuisho imeingizwa kwenye mtaala ili kuona walimu wote wanapotoka
vyuoni wana utaalama ya kufundisha wanafunzi wenye ulemavu.
Comments
Post a Comment