WATU WANNE WAFARIKI DUNIA KWA AJALI BARABARANI


 Watu wanne wameripotiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa kufuatia ajali  8  za  barabarani zilizotokea kwa mwezi  huu wa nane katika Mkoa wa Kusini Pemba.

Akizungmza na wandishi wa habari huko ofisini kwake madungu kamanda wa polisi Mkoa wa Kusini Pemba ASP Richad Tadei Mchovu amesema kati ya watu hao wawili walifariki katika ajali ya piki piki na wawili ni katika ajali mbili tofauti za gari.


Aidha amefahamisha kuwa ajali nyingi zinazotokea zinasababishwa na uzembe wa madereva, kwani wamekuwa wakitembea mwendo kasi.

‘’Ajali nyingi zinazotokea zinasababishwa na mwendo kasi walionayo madereva,’’ Alisema kamanda Mchovu.

Hivyo amewataka madereva kufuata sheria na taratibu za usalama wa barabarani wakati wanapoendesha vyombo vya moto,  jambo ambalo litaepusha ajali za kiholela.


Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO