NUHU KOMBO NUHU AENDELEA KUSOTA RUMANDE
NA FATMA HAMAD-- PEMBA.
Hatimae mahakama ya mkoa B Wete, imemrejesha tena
rumande mtuhumiwa wa ulawiti Kombo Nuhu Kombo miaka 19 baada ya kubainika kuwa
ni mtu mzima licha ya awali kupewa dhamana kama ni mtoto mahakamani hapo.
Awali mtuhumiwa alipelekwa rumande mwanzoni mwa mwaka
huu kwa tuhuma za ulawiti kwa kijana mwenye ulemavu wa akili ingawa upande wa
utetezi ulidai na kuthibitisha kuwa mteja wao hakutendewa haki kupelekwa
rumande kwa sababu ni mtoto.
Wakati kesi yake ikiendelea miezi mitatu iliyopita na kuwasilishwa vielelezo mahakamani hapo na upande wa
utetezi mahakamani iliridhia na kumpa
dhamana mtuhumiwa huyo kama mtoto.
Huku upande wa mashtaka ukiendelea kung’ang’ania kwamba mtuhumiwa ni mtu mzima, kisha
uliwasilisha vielelezo kadhaa ikiwemo cheti cha kuzaliwa cha mtuhumiwa na
mahakama kutengua uwamuzi wake wa awali juu ya umri wa mtuhumiwa.
Mwendewsha mashtaka katika shauri hilo Juma Ali Juma
alidai mahakamani hapo kuwa anaelewa kuwa mtuhumiwa Nuhu Kombo Nuhu ni mtu mzima na hakupaswa kupewa dhamana kwa
kisingizio cha kuwa ni mtoto.
Ndipo April 13 mwaka huu kesi hiyo ilisomwa tena upya
mbele ya hakimu Ali Abdulrahman Ali na kuamuru mtuhumiwa huyo kurejeshwa tena
rumande baada ya vielelezo vyake vilivyokubaliwa na kuonyesha kwamba ni mtu mzima.
“ April 5 mwaka huu baada ya kupokea vilelezo na
kujiridhisha juu ya umri wa mtuhumiwa dhamana yake imefutwa na sasa atarudi
tena rumande na kurejea tena mahakamani hapa April 27 mwaka huu kuendelea na
kesi yake” , alisema.
Awali mtuhumiwa huyo alipandishwa mahakamani hapo
akikabiliwa na tuhuma za kumlawiti kijana mwenye ulemavu wa akili mwenye miaka
19 jambo ambalo ni kosa kisheria
Tukio hilo lilitokea tarehe 13/ 12/ 2021 majira ya sa
moja asubuhi huko kijichame wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo
mtuhumiwa alimlawiti kijana mwenye ulemavu wa akili.
Ilidaiwa kuwa kufanya hyivyo ni kinyume na kifungu cha
116[1] cha sheria nambari 6/2018 sheria
ya Zanzibar.
Comments
Post a Comment