UDHALILISHAJI BADO NI KILIO KWA WANAWAKE NA WATOTO


 

NA FATMA HAMAD- PEMBA.

Mahakama  maalum inayoshughulikia kesi za udhalilishaji mkoa wa Kusini Pemba imeihairisha kesi ya ubakaji inayomkabili mtuhumiwa Ali Usi Simai mtumzima wa miaka 32 mkaazi wa Mchakwe Muambe anaedaiwa kumbaka msichana wa  miaka  nane (8)ambapo kufanya hivyo ni kosa kisheria.

Akizungumza mbele ya Mahakama hiyo mwendesha mashtaka wa Serikali kutoka Ofisi ya mkurugenzi  wa mashtaka DPP  Seif Mohd Khamis ,aliiambia mahakama  iihairishe kesi hiyo  kwani  upande wa mashtaka hawakupokea  chaji shiti  ya kesi wenyewe.

“Mheshimiwa sikupokea chaji shiti, kwa hivyo siwezi kucheza na haki ya mtu  kwani sijui kilichoandikwa kwenye file hilo naomba uipangie siku nyengine ili niweze kulipitia’’, alisema DPP Seif.

Kwa upande wake wakili wa kujitegemea Saleh Said Moh’d alisema hakubaliani na ombi hilo kwani  wamekuja na mashahidi 4 akiwemo  mwenyewe  mtuhumiwa, hivyo kuihairisha itakuwa shida lazima tuwaangalie  mashahidi wenyewe wametoka mbali jambo ambalo  kuja na kurudi itawaumiza.

Hakimu wa mahakama hiyo Muumin Ali Juma alisema amekubaliana na upande wa mwendesha mashtaka wa  Serikali kwamba hawezi kufanya utetezi kwani hajui kilichoandikwa kwenye file hilo, hivyo hatutoisikiliza kesi hiyo na itarudi tena tarehe 19/3  mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa.

Mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo ambapo ni kosa kinyume na kifungu cha 108 (1) (2) (e) na 109 (1) sheria nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibaer.

                        

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.