KUKOSEKANA MKALIMANI MASKULINI BADO NI TATIZO KWA WANAFUNZI WENYE ULEMAVU
NA FATMA
HAMAD-- PEMBA.
Kukosekana
kwa walimu wanaojua lugha za alama maskulini bado ni kilio kikubwa kinacho wa
kwaza wanafunzi wenye ulemavu kisiwani Pemba.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao Kwale gongo wilaya ya Wete kaskazini
Pemba, wazazi wa watoto wenye ulemavu walisema suala la kuchanganywa
darasa pamoja na wanafunzi wengine bila
ya kuepo kwa mwalimu wa lugha za alama
kunachangia wanafunzi hao kutofaulu mitihani yao na kusababisha kushindwa
kufikia malengo yao.
‘’Mfumo wa elimu
mjumuishi wa kuchanganywa pamoja na wanafunzi wenye ulemavu na wengine
bado hauja watendea haki watu wa aina hiyo maskulini,’’ alisema mama mzazi wa Abdala
Hussein mwenye ulemavu wa uziwi, mdomo na mguu.
Alisema
mtoto wake anasoma darasa la kumi ila hana tamaa ya kufaulu kutokana na
changamoto hiyo na kuiomba wizara ya elimu kumuona kijana huyo na kuweza kumsaidia kwa hali na
mali ili kuona na yeye amekuja na ufaulu mzuri.
Akiendelea kueleza kwa masikitiko mama huyo alisema kiukweli wanafunzi wenye ulemavu kitendo cha kwenda Skuli ni kwenda kupoteza muda tu ila lengo hasa la kusomana kufaulu halipo.
Kwa upande wake baba mzazi wa Salum Said Asaa mwenye ulemavu wa macho alisema kuwa yeye mtoto wake alishindwa kumpeleka skuli kwani anahisi ni kwenda kupoteza muda tu haoni anachokwenda kukisoma na kukifahamu.
‘’Mimi mtoto
wangu angalikuwa alishafika darasa la
pili ila nimeshindwa kumpeleka skuli kwani hakuna mwalimu wa kumfundisha yeye ,
bali namuacha ande chekechea tu ili
apoteze muda tu”, alieleza mama mzazi wa Salum.
Mzazi huyo
aliitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kufanya jitihada ya kujenga skuli
maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu ili kuona na wao wanasoma na kupata
ajira.
‘’Kwa kweli
wanafunzi wenye ulemavu huwa hatuwarejeshi tuna wapeleka mbele tu alimradi wamalize masomo yao wapumzike, ila
hawana wanacho kisoma na wala hawawezi kufaulu mitihani yao”, alieleza mwalimu
mkuu.
Alisema kwa
kweli matokeo ya wanafunzi wenye ulemavu ni mabaya, hivyo jitihada za makusudi
za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinahitajika ili kuona inasomesha walimu
wengi wa elimu mjumuishi.
Hata hivyo
alieleza kuwepo kwa mwalimu wa aina hiyo kunaweza kuwafanya wanafunzi
hao kupata vyema haki zao za msingi ya elimu na kuhakikisha wanafaulu mitihani yao na
kufikia upeo wa akili zao.
Comments
Post a Comment