Kukosekana kwa mkalimani maskulini kunadumaza mafanikio ya wanafunzi wenye ulemavu Pemba
Kukosekana
kwa walimu wanaojua lugha za alama maskulini bado ni kilio kikubwa kinacho wa
kwaza wanafunziwenyeulemavu kisiwani Pemba.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari hizi huko kijijini kwao Kwale gongo wilaya ya Wete kaskazini
Pemba, wazazi wa watoto wenye ulemavu walisema suala la kuchanganywa
darasa pamoja na wanafunzi wengine bila
ya kuepo kwa mwalimu wa lugha za alama
kunachangia wanafunzi hao kutofaulu mitihani yao na kusababisha kushindwa
kufikia malengo yao.
‘’Mfumo wa elimu
mjumuishi wa kuchanganywa pamoja na wanafunzi wenye ulemavu na wengine
bado hauja watendea haki watu wa aina hiyo maskulini,’’ alisema mama mzazi wa Abdala
Hussein mwenye ulemavu wa uziwi, mdomo na mguu.
Alisema
mtoto wake anasoma darasa la kumi ila hana tamaa ya kufaulu kutokana na
changamoto hiyo na kuiomba wizara ya elimu kumuona kijana huyo na kuweza kumsaidia kwa hali na
mali ili kuona na yeye amekuja na ufaulu mzuri.
Akiendelea
kueleza kwa masikitiko mama huyo alisema kiukweli wanafunzi wenye ulemavu kitendo cha kwenda Skuli ni kwenda kupoteza
muda tu ila lengo hasa la kusoma na kufaulu
halipo.
Kwa upande
wake baba mzazi wa Salum Said Asaa
mwenye ulemavu wa macho alisema kuwa yeye mtoto wake alishindwa kumpeleka
skuli kwani anahisi ni kwenda kupoteza muda tu haoni anachokwenda kukisoma na
kukifahamu.
‘’Mimi mtoto wangu
alishafika darasa la pili ila nimeshindwa kumpeleka skuli kwani hakuna mwalimu wa kumfundisha yeye , bali namuacha ande chekechea tu ili apoteze muda tu”, alieleza mama mzazi wa Salum.
Mzazi huyo
aliitaka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kufanya jitihada ya kujenga skuli
maalum kwa ajili ya watu wenye ulemavu ili kuona na wao wanasoma na kupata
ajira.
Nae mwalimu
mkuu wa Skuli ya Kinyasini iliyopo Wete Pemba Asha Mbarouk Rashid alisema kwa
kweli wanapata shida kufundisha wanafunzi wenye ulemavu kwani hawana taaluma
hiyo na wala hawana mwalimu hata mmoja anejua lugha ya alama.
‘’Kwa kweli
wanafunzi wenye ulemavu huwa hatuwarejeshi tuna wapeleka mbele tu alimradi wamalize masomo yao wapumzike, ila
hawana wanacho kisoma na wala hawawezi kufaulu mitihani yao”, alieleza mwalimu
mkuu.
Alisema kwa
kweli matokeo ya wanafunzi wenye ulemavu ni mabaya, hivyo jitihada za makusudi
za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinahitajika ili kuona inasomesha walimu
wengi wa elimu mjumuishi.
Hata hivyo
alieleza kuwepo kwa mwalimu wa aina hiyo kunaweza kuwafanya wanafunzi
hao kupata vyema haki zao za msingi ya elimu na kuhakikisha wanafaulu mitihani yao na
kufikia upeo wa akili zao.
Comments
Post a Comment