KAMATI ZA ULINZI NA USALAMA PEMBA ZA TAKIWA KUWA WADILIFU WAKATI WA UKODISHWAJI WA MASHAMBA YA MIKARAFUU
Kamati za
ulinzi na usalama katika mikoa miwili ya Pemba zimetakiwa kuwa makini katika kusimamia
zoezi la ukodishwaji wa mashamba ya karafuu ya Serikali ili kuona misingi ya
ukodishaji wa mashamba hayo inafuatwa na kuepusha upotevu wa mapato ya
serikali.
Akizungumza
katika kikao na kamati iliyoonda kusimamia ha ukodishwaji wa mashamba hayo Mkuu
wa Mkoa wa kaskazi Pemba Salama Mbarouk Khatibu amesema kamati hizo zinao
wajibu mkubwa wa kuona mashamba ya karafuu yanakodishwa katika hali ya amani
bila ya kuwepo na migogoro.
‘’Munadhamana
kubwa kuhakikisha hakutokei migogoro yoyote wakati wa zoezi hilo la ukodishwaji
mikarafuu’’ Alisema bi salama.
Amewafahamisha
kuwa endapo watasimamia zoezi hilo kwa uadilifu wa hali ya juu na kufuata taratibu zilizowekwa kutasaidia
kuiongezea Serikali mapato yanayotokana na zao la karafuu.
Mkuu wa wilaya ya Wete Mgeni Khatibu Yahya
ameziomba kamati za ulinzi na usalama kufuatilia maeneo ambayo tayari uchumaji
wa karafuu umeanza na kuhoji wapi zimechumwa .
‘’Nivyema mukapita panapoanikwa mukahoji, isjekua wanachuma katika yale mashamba ya Serikali yatakayo kodishwa’’ Alisema mkuu wa Wilaya
Wete
Mapema Afisa Mdhamini wizara ya kilimo, Umwagiliaji, Mali Asili na Mifugo Hakim Vuai Shein ameitaka kamati itakayo simamia zoezi la ukodishaji wa mashamba kufanya kazi kwa mashirikiano na wizara hiyo ili kuepusha malalamiko yanayojitokeza kama ilivyokua misimu uliyopita .
Serikali
kupitia Wizara ya Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo imekuwa na utaratibu
wa kukodisha mashamba ya karafuu kwa kila inapofika msimu na wakati mwengine
kumekuwa kukiibuka malalamiko ya wananchi na wakulima juu ya kutofuatwa kwa
utaratibu wakati wa ukodishaji wa mashamba hao.
Comments
Post a Comment