WIZI WA MBUZI WAMSABABISHIA KWENDA JELA PEMBA
NA FATMA HAMAD PEMBA 11/6/2021.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba limefanikiwa kuwakamata
watu 30 wanaotuhumiwa kujihusisha na
matukio mbali mbali ikiwemo wizi wa mazao pamoja na mifugo.
Akizungumza na Wandishi wa habari
huko ofisini kwake Madungu Kamanda wa
polisi mkoa huo Richad Mchovu amesema watuhumiwa hao wamewakamata kupitia
opereshen ya wiki moja iliofanywa na jeshi hilo Mkoani
hapa kwa ajili ya kupambana na uhalifu ambao wanafanyiwa wananchi katika Vijiji
vyao.
Amesema wahalifu hao 30, saba ni wezi wa mifugo, sita ni wezi wa mazao katika maeneo tofauti
, wawili ni wezi wa mbuzi, wanne walikamatwa maeneo ya mtambile wakiwa wameiba
ngombe 3, watatu walikamatwa na madawa ya kulevya na kumi
na mbili ni wizi wa kuku.
Amefahamisha kuwa mmoja wawili kati ya hao walioiba mbuzi tayari hatua
za kisheria zimeanza kuchukuliwa dhidi yake na ameshahukumiwa kutumikiwa chuo cha mafunzo.
Aidha amesema upareshen hiyo bado
inaendelea hivyo amewataka wananchi wanasafirisha mazao yao kupeleka sokoni
kuchukua vibali kwa sheha ili kuondokana na usumbufu bara barani jambo ambalo
litasaidia kuwakamata kwa urahisi wahalifiu wanaojishuhulisha na vitendo hivyo.
Kamanda mchovu ameoa wito kwa
Wananchi kushirikiana na jeshi hilo kuwafichua wahalifu na kuwapeleka vituoni ili
sheria ichukue naeasi yake jambo ambalo litapelekea kuishi kwa amani mitaani
mwao.
Comments
Post a Comment