Wawili washikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za wizi wa mifugo.
FATMA HAMAD FAKI - PEMBA.
Jeshi la
Polisi Mkoa wa Kusini Pemba linawashikilia vijana wawili wakituhumiwa kwa wizi
wa mifugo huko Kiwani na Mgagadu Wilaya ya Mkoani Mkoa wa kusini Pemba.
Kamanda wa
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Pemba ACP Richard Tadei Mchovu amewataja vijana
hao kuwa ni Moh`d Salum (35) Mkaazi wa Kilimani Mgagadu na Yussuf Rashid
Moh`d (30) Mkaazi wa Nanguji Kiwani
katika Wilaya ya Mkoani Pemba ambapo wamekamatwa afajiri ya jana June 21 wakiwa
na ng`ombe kwenye gari aina ya keri..
Akizungumza
na waandishi wa habari huko ofisini kwake Madungu Chake Chake Kamanda Mchomvu
amesema watuhumiwa hao wamekatwa na ng`ombe na wawili katika operesheni
iliyofanya na jeshi hilo la kudhibiti wizi wa mifugo.
Aidha
Kamanda Mchovu ametoa wito kwa wananchi kushirikiana pamoja katika kuzuia wimbi
la wizi wa mifugo ambalo limekithiri katika maeneo mbali mbali huku akitoa wito
kwa wafuagaji kuwa makini katika uangalizi wa mifugo yao.
Kwa upande
mwengine Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Pemba ACP Mchovu amesema jeshi hilo
pia limefanikiwa kukamata mifugo mengine mbali mbali ya wizi kwenye mkoa huo ikiwemo
ya mbuzi na kuku.
Jumla ya
kesi 10 za wizi wa mifugo zimeripotiwa tokea kuanzishwa kwa kampeni ya “Familia
yangu haina Uhalifu” ilionzishwa na jeshi la Polisi Mkoa wa kusini Pemba katika
kukabiliana vitendo vya uhalifu, ikiwemo, wizi, na udhalilishaji.
Comments
Post a Comment