WANDISHI WA HABARI WATAKA MABADILIKO KWENYE VIFUNGU VYA SHERIA AMBAVYO VINANYIMA UHURU WA HABARI

 

 NA FATMA HAMAD,PEMBA                                                                

Wandishi wa habari wametakiwa kutumia taluma yao kwa kuvisemea vipengele vilivyomo kwenye sheria za habari ambavyo vimekuwa vikiwandamiza wandishi pamoja na vyombo vya habari katika utekelezaji wa kazi zao ili viweze kurekebishwa.

Hayo yamesemwa na Shifaa Said Hassan kutoka baraza la Habari Tanzania [MCT] wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa wandishi wa habari kuhusu masuala ya habari yaliofanyika ukumbi wa TAMWA Mkanjuni Chake chake Pemba.

Alisema miongoni mwa vifungu ambavyo vimekuwa ni kikwazo kwa wandishi wa habari ni kifungu cha 4, na kifungu cha 27[1] vya sheria ya Usajili wa wakala wa habari Magazeti na vitabu No 5 ya mwaka 1988 iliyo rekebishwa na sheria no. 8 ya mwaka 1997.

Aidha aliendelea kufahamisha kuwa vifungu vengine ambavyo vimekua ni kikwazo kwa wandishi wa habari pamoja na vyombo vya habari ni kifungu cha 6 [1] na 7[1] vya sheria ya Tume ya Utangazaji No. 7 ya mwaka 1997 kama ilivyofanyiwa marekebisho na sheria No 1 ya mwaka 2010.

Alisema wandishi wa habari wananafasi kubwa katika jamii hivyo endapo watatumia taluma zao na nafasi zao walizo nazo na kuzisemea kunaweza kukapatikana kwa mabadiliko kwenye sheria hizo ambazo zimekuwa ni kandamizi.

‘’Nyinyi wandishi mna nafasi kubwa , hivyo mkiyasemea mapungufu hayo yanaweza yakarekebishwa na kupatikana kwa uhuru wa habari pamoja na vyombo vya habari,, alisema.

 Kwa upande wake Mwandishi wa habari mkongwe Haura Shamte amewataka wandishi wa habari kuzisoma na kuzifahamu Sheria za habari kwa usahihi wake jambo ambalo litawaepusha kujingiza katikamatatizo


.Nae Afisa mradi kutoka Chama cha Wandishi wa habari wanawake Tanzania Zanzibar [TAMWA]  Zaina Abdala Mzee amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha wandishi wa habari waweze kuvifahamu vifungu vya  sheria ambavyo vimekuwa ni kikwazo kwao na kuweza kuvisemea ili viweze kubadilishwa.



 


Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.