.KATIBU MKUU WA CHAMA CHA CUF AMEVITAKA VYAMA VYA SIASA KUITUNZA NA KUILINDA AMANI YA NCHI

 
 NA FATMA HAMAD, PEMBA.

Katibu Mkuu wa chama cha wananchi [CUF] Hamad Masoud Hamad amevitaka Vyama Vya Siasa kufanya siasa za kistarabu ili kuepusha maafa  yanayoweza kujitokeza katika Nchi.


Katibu huyo ameyasema hayo katika hafla ya kuwaombea duwa wafuasi wa chama hicho waliofariki katika Mandamano ya mwaka 2001  pamoja na wanzilishi wa chama hicho iliyofanyika Mchanga mdogo Wete Pemba.

Alisema maafa yakitokea hayachagui, hivyo ni vyema Viongozi wa vyama vya siasa kuendesha siasa zao kistarabu na kwa mujibu wa taratibu na sheria zinavyoelekeza ili kuepusha migogoro isiyoyalazima.

‘’Niwaombe viongozi wenzangu tujitahidi sana katika siasa zetu ili kilichotokea mwaka 2001 tuhakikishe hakitokei tena kwenye maisha yetu ni hatari, alisisitiza

Aidha aliitaka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuweka mkakati madhubuti ili kuona kila mmoja anaheshimu haki ya mwenzake, jambo ambalo litasaidia kuendelea kuwepo kwa Amani na Utulivu Nchini. 

 Kwa upande wake Mwenyekiti  wa Sughuli za Uhamasishaji wa Chama cha [CUF]  Pemba Rashid Ali Hamad amesema wananchi na wafuasi wa vyama ya siasa havipaswi kutofautiana katika kuwaombea dua wenziwao  hao ambao tayari walishatangulia mbele ya haki.

Alieleza kuwa imekuwa ni utaratibu kwa chama hicho kila ifikapo January 27 kufanya duwa hiyo kwa ajili ya kuwa kumbuka wenziwao waliofariki.

 Duwa hiyo imeandaliwa  na Chama cha CUF ilihusisha wananchi na wafuasi wa vyama vyengine vya siasa, walimu na wanafunzi  wa Madrasa za Qur-an kisiwani Pemba.

 

 

 

 

 

 

 


 



Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.