AFISA MDHAMINI WIZARA YA UTALII PEMBA ATOA NENO KWA WANDISHI WA HABARI


                                     NA FATMA HAMAD, PEMBA

Afisa mdhamini  wizara ya Utalii na mambo ya kale Pemba Zuhura Mgeni amewataka Wananchi  wa Pemba pamoja na wageni kutoka nje ya Pemba kuvitembelea vivutio vya Utalii vilivyopo kisiwani humo ili waweze kuitangaza Pemba kiutalii.

Akizungumza na Wandishi wa habari kutoka Chama cha wandishi wa habari [PPC] kisiwani Pemba  mara baada ya kumaliza  ziara ya kutembelea vivutio vya Utalii vilivyopo kisiwani humo.

Alisema kisiwa cha Pemba hususani mkoa wa kaskazini umejaliwa na vivutio vingi vya utalii, hivyo ni vyema wananchi pamoja na wageni kuvitembelea vivutio hivyo ili viweze kuinua Pemba katika Sekta ya Utalii.

‘’Niipongeze Jumuiya ya Wandishi wa habari Pemba kwa uwamuzi muliochukuwa wa kutembelea vivutio  mbali mbali vya  Utalii vilivyopo Pemba ili muweze kuutangaza utalii kisiwani humo,alisema.

Alisema sekta ya Utalii ni moja ya sekta ambayo inaisaidia Serikali kuingiza mapato, hivyo watahakikisha wanavitunza vivutio vya Utalii ili kuona uchumi wa Pemba umekua.

 Kwa upande wake mkuu wa wilaya  ya  Micheweni Mgeni Khatib Yahya amewataka wawekezaji kujitokeza kwa wingi ili waweze kujiekeza katika vivutio vilivyopo ndani ya wilaya  ya  Micheweni jambo ambalo litasaidia kukuza pato la Serikali.

 Baadhi ya wananchi kisiwani Pemba walisema kuwepo kwa vivutio vya utalii kumewanufaisha kwani kumewasaidia Vijana wengi kupata ajira.

 Nae katibu wa Jumuiya ya Wandishi wa habari [ PPC]  Bakar Mussa Juma alisema lengo la kutembelea  vivutio vya Utalii vilivyomo kisiwani humo ni kuunga mkono juhudi za  Serikali ya Mapinduzi za kuutangaza Utalii  katika kisiwa cha Pemba.

 

 

 

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.