MIUNDO MBINU MIBOVU YA SKULI YA PUJINI KERO KWA WANAFUNZI SKULINI HAPO

 
 NA FATMA HAMAD, PEMBA

Walimu wa Skuli ya msingi Pujini wilaya ya Chake chake mkoa wa Kusini Pemba wametoa ya moyoni juu ya uwepo wa  miundombinu mibovu, pamoja na uhaba wa madarsa ya kufundishia Wanafunzi wao.

Wakizungumza mbele ya viongozi wa jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Chake chake wamesema baadhi ya madarsa yanavuja jambo linalopelekea kipindi cha mvua kushindwa kuendelea na vipindi kutokana na kukosa sehemu ya kufundishia.

,,Tunakilio Skuli yetu inavuja ikinyesha mvua inabidi tutafute sehemu tujifiche mpaka mvua ipite ndio tuendelee na vipindi, walieleza.

Aidha walisema kuwa bado wanachangamoto ya uhaba wa vyumba vya kufundishia, hivyo wanahitaji kusaidiwa kuezekewa jingo lao ambalo tayari walishalijenga.

Badhi ya wanafunzi wanaosoma Skulini hapo wamesema darasa moja lina zaidi ya wanafunzi 80,hivyo wameutaka uongozi huo kuwafanyia msaada wa kuwezekea pamoja na kuwajengea madarasa mengine jambo ambalo litaondosha usumbufu kwa wanafunzi pamoja na walimu wao.

,,Hatufahamu vizuri tukisomeshwa, kwani Tunakuwa tuko wengi kutokana na ufinyu wa madarasa,walieleza.

 Aidha walitaka Serikali ya Mapinduzi kuendelea  kutoa Mabuku maskulini jambo ambalo litasaidia hata wenye hali ngumu kupata haki yao ya Elimu.

Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza kuu la jumuiya ya Wazazi Taifa Juma Othman amewataka Wanafunzi hao kutoa tarifa kwa Walimu au Wazazi wao pindi kunapotokea vitendo vya udhalilishaji ili viweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

 Nae mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Chake chake Abdul Aziz Omar Juma amesema lengo la kufanya ziara ya kutembelea Skuli na kusikiliza Kero zilizopo na kuzichukuwa ili ziweze kutatuliwa.

 Ziara hiyo ilifanyika katika Skuli ya Pujini, Wesha, DK Mpango pamoja na Uzalendo zote zilizopo katika wilaya ya Chake chake ikiwa ni shamra shamra ya madhimisho ya kuzaliwa kwa Chama cha Mpinduzi.


 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.