Waandishi wa Habari Pemba Watakiwa kutoa elimu kwa vyama vya siasa juu ya nafasi ya mwanamke.
Wandishi
wa habari wametakiwa kutoa elimu kwa vyama vya siasa waweze kutoa fursa sawa za
uongozi kwa Wanawake na Wanaume ili kuona Wanawake na wao wanashika nafasi za uongozi
katika ngazi mbali mbali za maamuzi.
Hayo
yamesemwa na mwezeshaji wa mafunzo ya uhamasishaji wa Wanawake katika ushiriki wa
Demokrasia na uongozi kwa wandishi wa habari huko Ofisi za Tamwa Mkanjuni Chake
chake Pemba.
Amesema
imeonekana bado hakuna uwiano sawa baina ya wanaume na Wanawake katika ngazi mbalimbali
za maamuzi, hivyo ni jukumu la wandishi wa habari kuwa eilimisha viongozi wa vyama
vya siasa kuondosha vikwazo ambavyo vinawakosesha fursa ya uongozi wanawake wenye
nia ya kugombea.
‘’Ni
jukumu lenu Wanahabari kuwapa elimu viongozi wa kisiasa kuondosha vikwazo vinavyowafanya
wanawake washindwe kuwa viongozi’’. Alisema Bi sabah.
Amesema
mwanamke ana nafasi kubwa ya kuwasilisha matatizo ya jamii yakiwemo ya Wanawake
katika vyombo vya mamuzi kwa kulinganisha naWanaume.
Hivyo
ameisihi jamii kuondosha dhana potofu na badala yake waone kwamba mwanamke na yeye
anaweza kuwa kiongozi.
Hadia
Faki Juma mshiriki wa mafunzo hayo amesema mfumo dume uliopo kwa vyama vya siasa
pamoja na jamii umekuwa ukiwakatisha tama wanawake walio na nia ya kugombea.
Nae
Suleiman Rashid Omar ambae pia ni mshiriki wamafunzo hayo amesema ni vyema Wanawake
kulipa kipao mbele suala la Elimu jambo ambalo litawajengea uwezo wanawake wakati
watakapopata fursa za uongozi.
Mafunzo
hayo ya siku nane kwa wandishi wa habari yameandaliwa na chama cha wandishi wa habari
wanawake Zanzibar Tamwa, Zafela pamoja na Pegao kwa kushirikiana na Ubalozi
wa Norway Nchini.
Comments
Post a Comment