VIONGOZI WA DINI WAHIMIZWA KUTOA ELIMU KWA JAMII JUU YA UMUHIMU YA MWANAMKE KUWA KIONGOZI
Viongozi wa
dini wana nafasi kubwa ya kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa mwanamke kushika nafasi za ungozi
katika ngazi mbali mbali za kutunga Sheria.
Akizungumza
na viongozi wa dini ya kiislamu Kisiwani Pemba
Afisa fatwa kutoka ofisi ya Mufti Sheikh Said Ahmad Muhammed katika
mkutano wa uwasilishwaji wa ripoti ya miezi mitatu juu ya mwanamke kuwa
kiongozi huko Tamwa Chake chake Pemba.
Sheikh Said
alisema Uislamu hauja mkataza mwanamke kua kiongozi ilihali tu afuate
Sheria,Mila na Maadili yake .
‘’Dini
haijamzuia mwanamke kuwa kiongozi bali afuate sheria na Madili ya dini yake’’
Alisema Sheikh Said.
Hivyo
alisema wakati umefika kwa viongozi wa dini mbali mbali kutoa elimu kwa jamii
ili kuhakikisha mwanamke nayeye anashiriki katika nafasi mbali mbali za
uongozi.
Aidha Shikh
Said amewataka wazazi na Walezi kutowabagua watoto Kijinsia
katika kutoa fursa za kuwapatia Elimu.
Wakichangia
katika mkutano huo baadhi ya viongozi hao
walisema kuwa ipo haja ya kutolewa elimu kwa Masheikh na maimu pamoja na
wanajamii ili kufahamu kwamba mwanamke nayeye
anaweza kuongoza.
Comments
Post a Comment