‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’
NA FATMA HAMAD, PEMBA Katibu mkuu wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Khamis Abdala Said amewataka wandishi wa habari kuielimisha jamii kufahamu umuhimu wa malezi na makuzi ya awali ya mtoto, ili kufahamu utaratibu wa kuwalea katika kipindi hicho, na kupatikana kizazi chenye afya njema. Alisema katika visiwa vya Zanzibar bado kuna tatizo la udumavu kwa watoto kutokana na kukosa huduma muhimu kama vile Afya, Chakula bora, ulinzi pamoja na ushirikishwaji, hasa katika kipindi cha awali cha malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto. Katibu Mkuu huyo aliyasema hayo wakati akifunga mafunzo ya siku nne Waandishi Vinara wa ECD Zanzibar, yaliofanyika Mjini Dar esalam. Alisema wandishi wa habari wanajukumu kubwa katika jamii, hivyo ipo haja kuwaelimisha kufahamu umuhimu wa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto, ili kupata kizazi chenye madili na afya bora. ‘’Ndugu zangu wandishi wa habari nyinyi mnadhima kubwa ka...
Comments
Post a Comment