Bidhaa zenye Viwango ndio chanzo cha maendeleo kwa Wajasiriamali.





 

Wajasiriamali Kisiwani  wametakiwa  kuzalisha Bidhaa  zenye  ubora na zenye  Viwango  ili kupata Soko la ndani na nje ya Nchi.

Hayo yamesemwa na Afisa Mdhamini wizara ya Biashara Viwanda na Masoko Ali Suleiman wakati akizungumza na Wajasiriamali huko ukumbi wa Chama cha Wandishi wa habari Wanawake Tanzania Zanzibar Mkanjuni Chake chake Pemba.

Amesema iwapo biashara hizo zitakuwa na kiwango kinachostahiki kutawasaidia bidhaa zao kupata Soko la uhakikia.

Amesema  sasa hivi Ulimwengu uko katika mabadiliko ya Kidijitali, hivyo ni vyema wajasiriamali waendane na mabadiliko hayo waweze kuzalisha bidhaa ambazo zitaweza kuwapatia tija.

Aidha amesema Changamoto kubwa ya Wajasiriamali ni ukosefu wa Masoko ya kuuzia bidhaa zao, hivyo wakizalisha biashara zenye viwango watauza katika masoko ya Afrika Mashariki.

Alifahamisha kuwa endapo wataweza kuzalisha biashara zenye viwango watapata wateja kwa wingi na kukuza uchumi wao na kuondokana na hali ngumu ya maisha.

















 

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.