Umaskini ni moja ya chanzo za udhalilishaji.


 

UMASKINI uliokithiri  imebainika kuwa  ni moja ya  sababu inayopelekea  Watoto   kufanyiwa  Udhalilishaji.

Hayo yamesemwa na mdau wa mtandao wa kupinga udhalilishaji kutoka Wilaya ya Mkoani, katika mkutano wa uwasilishaji wa ripoti za utekelezaji wa majukumu yao ya kutoa elimu  juu ya madhara ya udhalilishaji wa kijinsia kwa jamii uliofanyika ofisi ya TAMWA Pemba.

Kwa upande wake Shaaban Juma Kassim Msaidizi wa sheria kutoka  shehia ya Mkanyageni, alifahamisha  kuwa udhalilishaji unafanyika zaidi kwa watoto  wanaokosa  malezi  ya  pamoja  ambao wazazi wao wameachana.

Alisema  takribani  watoto  wengi ambao wazazi wao wameachana, wanakosa masomo na badala yake wanatumikishwa ili wapate mahitaji yao  hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya watoto.

‘’Wanawake wengi hususan wanaoishi vijijini ni maskini, hivyo hushindwa kuwalea watoto ipasavyo na kupelekea kudhalilishwa’’,alisema Shaaban.

Nae Afisa Tathmini na ufuatiliaji wa chama cha Wandishi wa habari Wanawake  Zanzibar  Mohamed Khatib Mohamed, amewataka  wadau hao waendelee kuzifuatilia kesi, ambazo wameziibua  wakati walipokuwa wakitoa elimu.

Comments

Popular posts from this blog

UTELEKEZAJI WA WANAWAKE UNAVYOKATISHA NDOTO ZA WATOTO.

Mkuu wa Polisi Jamii Kaskazini Pemba akerwa na wanao wafungia ndani watoto wenye ulemavu.

Mrajisi wa Mahakama Zanzibar ahidi kula sahani moja na Mahakimu wasio wadilifu.