Posts

KIRARE BADO AISOTEA RUMANDE

Image
  FATMA HAMAD PEMBA. Mahakama ya mkoa B iliopo Kusini Pemba imeghairisha kesi ya kuingilia kinyume na maumbile inayomkabili kijana Khamis Abdala Khamis marufu kirare mwenye umri wa [20] mkaazi wa Kangani wilaya ya Mkoani baada ya mtuhumiwa huyo kukataa kusomewa shitaka lake . Kijana huyo wakati akiwa ametulia kizimbani na kusubiri asomewe shitaka lake aliambia mahakama hiyo kuwa hali yake sio mzuri anaomba kesi ighairishwe na ipangiwe siku nyengine. ‘’Mheshimiwa hakimu leo naumwa siwezi kukakaa hivyo naiomba mahakama yako ighairishe shauri hilo kwa leo’’ alieleza mtuhumiwa kirare. Hakimu wa mahakama hiyo Muumin Ali Juma   amesema hii ni mara ya pili unasema unaumwa   daktari anakuja na kurudi ila ujue baadae fursa hii hutoipata tena nitakua sikusikilizi tena , na mahakama itatoa oda ya kumruhusu daktari afanye shughuli zake mpaka utakapo kuwa tayari   ndio tutamleta na wewe   utarudi rumande hadi tarehe 9/ 8 2022kwa ajili ya kusikiliza ...

AFUNGWA JELA KWA KUTOROSHA MSICHANA

Image
  NA FATMA HAMAD PEMBA. Hatimae kijana  Ramadhan Khamis Mohd  mwenye umri wa miaka 19 mkazi wa Tironi  Mkoani Pemba  anza  maisha  mapya  ya kutumikia chuo cha Mafunzo kwa muda  wa miaka 5 baada ya kutiwa  hatiani  kwa kosa  la  kutorosha  msichana  wa  miaka  16. Baada ya kijana huyo kupanda kizimbani na kusubiri asomewe hukumu yake Mwendesha mashtaka  wa Serikali Mussa Khamis amemuambia  hakimu anaendesha kesi hiyo kuwa kesi iko kwa ajili ya kutolewa uwamuzi hivyo wao hawana pingamizi kama mtuhumiwa yuko tayari basi asomewe huku yake. ‘’Kama mtuhumiwa yuko tayari basi na sisi hatuna tatizo nivyema  asomewe hukumu yake ili ajue hatma yake’’ alieleza  DPP Mussa. Hakimu wa mahakama ya mkoa B  iliyopo Chake chake  Muumin  Ali Juma   alisema jumla ya mashahidi 4 walisikilizwa mahakamani hapo akiwemo muathirika mwenyewe na Mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa huyo....

ALIEDAIWA KUWA NI BUBU SASA AANZA KUSEMA

Image
  NA FATMA HAMAD PEMBA. Hatimae  Mahakama  ya  mkoa  B  Wete  yanza kusikiliza kesi ya ulawiti inayomkabili kijana  Nuhu Kombo Nuhu  miaka 19  mkaazi wa Kijichame wilaya ya Micheweni mkoa wa Kaskazini Pemba. Mwendesha mashtaka wa Serikali Juma Mussa Omar amemuambia hakimu anaendesha  kesi hiyo kuwa shauri hilo lipo kwa ajili ya kusikilizwa na tulikua tunasubiri  cheti  kutoka kwa mtaalamu wa Afya kuthibitisha kwamba kijana huyo ni mgonjwa hawezi kuzunguza  ama ni kiziwi. ‘’Mheshimiwa hakimu tulitoa ombi  mahakama yako impeleke  hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi  kama tayari basi tupo tayari kwa ajili ya kuskila’’ alisema DPP Juma. Hakimu wa  Mahakama hiyo Abdulrahman  Ali  ameleza  kuwa  tayari tumesha pokea uthibitisho kutoka  Hospitali na majibu hayakuonesha  kwamba  mtuhumiwa  huyo  ana  ugonjwa wowote. ‘’Majibu yanaonesha kwamba si kibu...

NUHU AENDELEA KULA BATA RUMANDE

Image
  NA FATMA HAMAD Pemba.  Mahakama   ya mkoa   B iliyopo   Wete   imeghairisha   shauri   la   Ulawiti   linalo mkabili   kijana   Nuhu Kombo   Nuhu   mwenye   umri   wa   miaka 19   mkazi   wa   Kijichame   wilaya   ya   Micheweni   Mkoa   wa Kaskazini   Pemba baada ya mtuhumiwa kudai   kuwa anaumwa na homa. Mtuhumiwa huyo     ameiambia mahakama hiyo kuwa hajisikii vizuri anaumwa hivyo anaiomba   kughairisha shauri hilo na apangiwe siku nyengine kwa ajili ya kusikilizwa. Mwenedesha mashtaka wa Serikali kutoka ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka DPP Juma Mussa Omar   amewambia mashahidi waliofika kwa ajili ya kutoa   ushahidi   wao kwamba mtuhumiwa leyo kasema anaumwa hivyo tukiendelea   tutakua tunamnyima haki yake . ‘’Kwa vile mtuhumiwa kasema hayuko vizuri nawaomba murudi na musichoke muje tena siku mutakayoitwa’’...

WEZI WA KARAFUU WATAKIONA MKUU WA MKOA ASEMA

Image
  NA FATMA HAMAD PEMBA. Serikali ya mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama   mkoani humo imesema hawatomvumilia mtu yoyote atakaefanya   vitendo vya   uhujumu    wa zao   la karafuu katika msimu   wa mwaka huu. Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya micheweni Mgeni Khatib Yahya   kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kaskazini pemba Salama Mbarouk Khatibu   mbele ya Masheha pamoja na wakulima wa   karafuu mkoa huo   huko jamuhuri Holl Wete Pemba. Amesema   wakati wa msimu wa karafuu   wapo watu   wanafanya ubabaishaji ikiwemo ununuaji   karafuu za vikombe   pamoja na uzwaji   wa karafuu chafu katika vituo vya ZSTC. ‘’Niwambie wezee wenzangu haipendezi kuonekana kwamba karafuu inanunuliwa na mchanganyiko wa uchafu tunaona aibu kama sisi viongozi, hivyo kwa msimu huu hatutokua tayari kuliona hilo tutahakikisha tumewafichua wote watakaofanya hivyo’’ alieleza mkuu wa mkoa. ...

WAKULIMA WA KARAFUU MKOANI PEMBA WA NENA.

Image
  NA FATMA HAMAD PEMBA. Wakulima wa zao la karafuu  wilaya ya Mkoani wameliomba shirika  la biashara la ZSTC  kuweka mikakati madhubuti  ili waweze kuwadhibiti wale wote  wanao jishuhulisha na biashara ya  ununuzi wa  karafuu   mbichi.  Wamesema uwepo wa watu wanao nunua karafuu mbichi za vikombe ni moja  ya sababu kubwa inayochangia  ongezeko la wizi  wa  zao hilo. Ushauri huo wameutoa katika mkutano wa  tathmini juu ya zao la karafuu katika msimu  wa mwaka huu huko Zstc Mkoani wamesema asilimia kubwa ya wanaoiba karafuu wanaziuza kwa wale wanao nunua karafu za vikombe, hivyo ni vyema watendaji wa Zstc kuwa makini na watu hao ili kuepusha uharibifu, pamoja na wizi  katika msimu wa mwaka huu. ‘’Mheshimiwa mkuu wa mkoa kweli tunaumizwa tunaibiwa karafuu zetu na hawa wanunuzi wa karafuu za vikombe ndio wanaosababisha tunaomba hilo mliangalie’’ walieleza wakulima. Kwa upande wake mkulima Zubei...

MTUHUMIWA AKATAA SHITAKA

  NA FATMA HAMAD PEMBA. Mahakama  ya  mkoa B iliopo   Kusini Pemba  imeghairisha  kesi ya  kuingilia kinyume na maumbile   inayomkabili   kijana  Khamis  Abdala Khamis  marufu   kirare   mwenye  umri   wa   [20] mkaazi  wa  Kangani  wilaya ya Mkoani   baada ya mtuhumiwa huyo  kukataa kusomewa shitaka lake .   Kijana  huyo wakati akiwa  ametulia  kizimbani  na  kusubiri  asomewe  shitaka  lake  aliambia mahakama  hiyo kuwa hali yake sio mzuri  anaomba  kesi ighairishwe na ipangiwe  siku nyengine.  ‘’Mheshimiwa hakimu leo naumwa   siwezi kukakaa hivyo  naiomba mahakama yako  ighairishe shauri  hilo kwa leo’’ alieleza  mtuhumiwa  kirare. Hakimu wa mahakama hiyo  Muumin  Ali  Juma hakufurahishwa na kauli  hiyo  na kumueleza   mtuhumiwa  huy...