NA FATMA HAMAD PEMBA Licha ya jitihada ya serekali ya mapinduzi ya Zanzibar katika ujenzi wa barara za lami bado kunawananchi ambao wamekuwa wakijenga karibu na miundombinu hiyo jambo ambalo likileta usumbufu kwa serekali Azikizungmza na wananchi wa wilaya ya micheweni mara baada ya uwekaji wa jiwe la msingi bara bara ya maziwangombe naibu sipika wa baraza la wakilishi Zanzibar Mgeni Hassani Juma amesema wapo baadhi ya watu wamekuwa wakijenga pembezoni mwa bara bara jambo ambalo limekuwa likigharimu serekali kwa kulazimika kulipa fidia wakati wa utanuzi wa miundombinu hiyo Hata hivyo amewataka watendaji wa wizara ya mawasiliano kulisimamia ili kuepusha malalamiko ambayo yanaweza kujitokeza kwa wananchi Mkuu wa mkoa kaskazini Pemba Salama Mbaruku Khatibu amesema ujenzi wa bara bara hiyo itatowa furusa kubwa kwa wawekezaji wanaotaka kuja kuwekaza katika maeneo huru ya micheweni Akitowa taarifa ya kitaalamu katibu mkuu wiazara ujenzi masiliano na uchukuzi Amori Hamili Bakari amesema...
Posts
JAMII YAHIMIZWA KUITUNZA AMANI
- Get link
- X
- Other Apps
NA FATMA HAMAD PEMBA. Wadau waliopatiwa mafunzo ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya mani wamehimizwa kuendelea kuielimisha jamii kujiepusha na migogoro isiyo ya lazima ambayo itapelekea uvujifu wa amani Nchini. Akizungumza na wadau waliopatiwa mafunzo ya utatuzi wa migogoro kutoka Tasisi mbali mbali Kisiwani Pemba Afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka kituo cha huduma za Sheria Zanzibar Khamis Haroun Hamad amesema badojamii imekabiliwa na migogoro mbali mbali hivyo ipo haja kuendelea kutolewa kwa elimu ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani ili kuona wanasuluhishana wenyewe kwa wenyewe bila ya kuekeana visasi. ‘’Migogoro ya Ardhi pamoja na ndoa imeonekana kwamba ndio inayoshamiri katika jamii hivyo ipo haja kwa wadau hao kuchukua jitihada za makusudi kuielimisha jamii kuchukuwa hatua stahiki pindi unapotokezea mgogoro jambo ambalo litasaidia kuepusha mivutano na mifarakano kwao’’ alisema Afisa ufuatiliaji. Aidha am...
MELI KUBWA LA WATALII KUTOKA UFARANSA LATUA KISIWANI PEMBA.
- Get link
- X
- Other Apps
NA FATMA HAMAD PEMBA. JUMLA ya watalii 69 wamewasili kisiwani Pemba kwa meli maalumu, kwa lengo la kujionea vivutio mbali mbali vya utalii vilivyomo Kisiwani humo. Watalii hao raia wa Ufaransa wamewasili Kisiwani Pemba kwa ziara ya siku Moja, kwa kutumia Usafiri wa meli aina ya LE BELLOT, wameweza kutembelea na kujionea vivutio vya utalii. Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuwapokea watalii hao, kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Kusini Pemba, Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Khatib Juma Mjaja, alisema ujio wa watalii hao ni kukitangaza kisiwa cha Pemba kiutalii kupitia vivutio mbali mbali vilivyomo. Alisema ujio wao utaweza kuwanufaisha wafanya biashara na wajasiriamali, kuuza na kutangaza bidhaa na biashara zao kimataifa. “Kwa sasa ni wazi kuwa Kisiwa cha Pemba kimeanza kufunguka kiutalii, ujio wao utaweza kuonyesha dunia kuwa Pemba kuna vivutio vingi vya Kiutalii, Pemba ni sehemu salama ya watalii kutembea”alisema. Aidha Mkuu huyo alisema ni meli ya pili h...
ATIWA MBARONI AKIDAIWA KUMLAWITI MLEMAVU WA AKILI
- Get link
- X
- Other Apps
Msifunzwa ni mamae hufunzwa ni ulimwengu hii imekuja baada ya Nuhu Kombo Nuhu mwenye mumri wa miaka 22 akihemea polisi kwa tuhuma za kumlawiti kijana wa 18 mwenye ulemavu wa akili na mdomo. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mama mzazi wa kijana huyo amesema ailikua yupo nae nyumbani badae akatoka na hakurudi tena na alianza kumtafuta ila hakumuona. Alisema kuwa baada ya muda mrefu kupita aliletewa nyumbani na msamaria mwema na kumuambia huyu mtoto wako nimemkuta Vichakani akiwa anafanyiwa udhalilishaji na Nuhu Kombo Nuhu. Alifahamisha kuwa baada ya hapo aliendelea kumuhoji na kumuambia kuwa hii ni kawaida yake kumchukua na kumpeleka vichakani kumfanyia kitendo hicho ‘’Nilipo muhoji aliniambia ashazoea kunifanyia hivi na ananiambia atanipa pesa na simu ya tachi’’ alieleza mama mzazi. Aidha mama huyo alisema kuwa baadhi ya wanafamili wa mtuhumiwa huyo wamekua ...
JAMII YAHIMIZWA KUWATUNZA NA KUWATHAMINI WATU WENYE ULEMAVU.
- Get link
- X
- Other Apps
kikundi Cha Mazoezi ya viungo cha Gombani Fitnes Senter kilichopo chake chake kimemtembelea na kumfariji kijana Asaa Khamis mwenye ulemavu wa Viungo Mkaazi wa Shumba ya Vyamboni wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba kufuatia habari iliyorushwa katika Blog ya Pemba ya leo iliyo muhusu kijana huyo akihitaji msaada wa kupatiwa mtaji kwa ajili ya kuendeleza biashara zake. Akizungumza mara bada ya kumfariji kijana huyo katibu wa Kikundi hicho Khalfan Amour Mohd alisema mbali ya kukindi hicho kufanya mazoezi pia kimekua kikifanya harakati mbali mbali za kijamii kama vile kusaidia watu wenye ulemavu, pamoja na kupiga vita masuala ya udhalilishaji hususan kwa walemavu . ‘’Unajua sisi tumeguswa na makala iliyorushwa kwenye mtandao inayomzungumzia Kijana Asaa jinsi anavyopata shida kutokana na ulemavu wake tukaona ipo haja ku...
WALIMU MASKULINI WAHIMIZWA KUJIONGEZA KIELIMU
- Get link
- X
- Other Apps
Afisa Elimu Wilaya chake chake Burhani Khamis Juma kwa niaba ya Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba amewataka Walimu wa skuli mbali mbali kisiwani Pemba kuitumia teknolojia ya mitandao ya kijamii ili waweze kujifunza na kuwafundisha wanawafuzi katika kuleta mabadiliko katika sekta ya Elimu. Afisa Elimu Wilaya chake chake Burhani Khamis Juma kwa niaba ya Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Afisa huyo Ameyasema hayo katika hafla ya kukabidhi vyeti kwa walimu waliohitimu mafunzo ya Elimu Mtandao na Masafa kutoka taasisi ya [SHAIBU FOUNDATION ] Chake Chake Pemba . Amesema kupitia mafunzo hayo ya elimu mtandao yatatoa fursa kwa walimu kuwajengea uwezo wa kuitumia mitandao katika kutafuta ...
WADAU MBALI MBALI WASHAURIWA KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA ILI KUMALIZA UDHALILISHAJI.
- Get link
- X
- Other Apps
NA FATMA HAMAD PEMBA. Mkuu wa Mkoa wa kusini Pemba Mheshimiwa Matar Zahor Massoud amesema Kuna ulazima wa kila mdau kushiriki kwa pamoja katika kusimamia Sheria na kanuni za kesi za udhalilishaji Ili kuiokoa Jamii kuondokana na majanga ya ukatili na udhalilishaji nchini Akizungumza kwa niaba ya Mkuu huyo wa Mkoa , Mkuu wa Wilaya ya Wete Dr Hamad Omar Bakar huko uwanja wa Mshaame Mata Micheweni katika maadhimisho ya siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia yaliyoandaliwa na Jumuiya inayopingana na ukatili na udhalilishaji wa kijinsia TUJIPE amesema udhalilishaji umekuwa kikwazo Cha kuleta maendeleo kwa wanawake na watoto hivyo Ili kuisaidia juhudi za Taifa katika kutokomeza janga Hilo ni budi kwa kila mmoja kuendelea kusimamia jukumu alilopangiwa Mapema mratibu wa jumuiya inayopingana na ukatili na udhalili Shaji wa kijinsia ya Tumaini Jipya (TUJIPE) Tatu Abdallah Mselem amesema licha kuwepo kwa Sheria na hukumu zinazotokewa katika watendaji wa matendo hayo Bado ud...