JAMII YAHIMIZWA KUITUNZA AMANI
NA FATMA HAMAD PEMBA.
Wadau waliopatiwa mafunzo ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya mani wamehimizwa kuendelea kuielimisha jamii kujiepusha na migogoro isiyo ya lazima ambayo itapelekea uvujifu wa amani Nchini.
Akizungumza na wadau waliopatiwa mafunzo ya utatuzi wa migogoro kutoka Tasisi mbali mbali Kisiwani Pemba Afisa ufuatiliaji na tathmini kutoka kituo cha huduma za Sheria Zanzibar Khamis Haroun Hamad amesema badojamii imekabiliwa na migogoro mbali mbali hivyo ipo haja kuendelea kutolewa kwa elimu ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani ili kuona wanasuluhishana wenyewe kwa wenyewe bila ya kuekeana visasi.
‘’Migogoro ya Ardhi pamoja na ndoa imeonekana kwamba ndio inayoshamiri katika jamii hivyo ipo haja kwa wadau hao kuchukua jitihada za makusudi kuielimisha jamii kuchukuwa hatua stahiki pindi unapotokezea mgogoro jambo ambalo litasaidia kuepusha mivutano na mifarakano kwao’’ alisema Afisa ufuatiliaji.
Aidha amesema bila ya kuepo kwa amani hakuna maendeleo yoyote hivyo amewasa wanajamii kuifanyia kazi elimu hiyo wanayopewa na kuepuka viashiria ambavo vinaweza vikasababisha kutoweka kwa amani iliyopo.
Nao wadau hao wameiomba Serikali ya mapinduzi Zanzibar kupunguza gharama za upatikanaji wa hatimiliki ili kila mtu aweze kumudu kuinunua jambo ambalo litaepusha kutokea kwa migogoro kwa jamii.
Comments
Post a Comment