Posts

MARYAM ALI: MGOMBEA UWAKILISHI ANAEPANIA KUMALIZA KERO ZA JIMBO LA MTAMBWE

Image
NA FATMA HAMAD, PEMBA Maryam Ali Rashid ni mgombea wa Chama cha Mapinduzi CCM, anaewania uwakilishi jimbo la Mtambwe. Binti huyu anaweka historia ni mfano tosha kwa wanawake, kwani amekua na uthubu wa  kuingia kwenye kinyan’ganyiro cha kusaka Jimbo akiwa bado ana umri mdogo, ana miaka 34.   Ameanza kushiriki katika shughuli za kijamii kupitia vikundi vya wanawake na miradi ya maendeleo kijijini kwao, maji elimu ya watoto na uwezeshaji wanawake hapo ndipo alipoanza kuingizwa zaidi kwenye siasa za chama kwa sababu kazi zake zinaonekana. ‘’Nimeanza kwa kutetea shida ya maji kijijini kwangu, ambayo imekua inawakwaza wananchi  kwa muda mrefu, na nimefanikiwa na sasa shida imeondoka,’’anasema.  Baada ya kuona matokeo hayo watu wakanza kumuomba aingie kwenye uongozi, afike kwenye ngazi za juu, aendelee kuwatetea. NAFASI AMBAZO AMEWAHI KUSHIKA KABLA YA KUGOMBEA Kabla ya kugombea uwakilishi Maryam alishika nafasi mbalimbali za kijamii na ndani ya chama katika ngazi ya shehia ...

SAFARI YA WANAWAKE WENYE ULEMAVU KUELEKEA UONGOZI

Image
                          NA FATMA HAMAD,PEMBA Kadri Tanzania inavyoelekea katika uchaguzi Mkuu kunakua na mijadala mingi kuhusu ushiriki wa makundi maalum hasa Wanawake Wenye Ulemavu.   Kwani ni muda mrefu kundi hili linakuwa likipigania nafasi sawa katika siasa, uongozi na maamuzi, safari yao inaendelea kuwa yenye milima na mabonde, ingawa mwakahuu inaonesha matumaini. Nasra Fakih Hassan mwanamke mwenye ulemavu wa mguu    mzaliwa wa Kangagani Wete Pemba , ambaye amejitosa kugombea nafasi ya uwakilishi viti maalumu, anasema mchakato wa uchaguzi umewaonesha matumaini, ingawa bado unahitaji mageuzi kwa watu wenye ulemavu ‘’Mara hii tunashukuru na ndio maana wanawake wengi wenye ulemavu tumejitokeza kuchukua fomu na kuwania nafasi mbali mbali za uongozi, ingawa si hayo tu bali hata kwenye kampeni tunashiriki kwa wingi na kusikiliza sera za wagombea,’’anasema. Nasra anabainisha kuwa, licha ya changamo...

ASHA MOH’D ALI MWANAMKE MWENYE NDOTO YA MABADILIKO

Image
  NA MOZA SHAABAN,PEMBA NATAMANI  moja niwe kiongozi nilete mabadiliko katika Jimbo langu. Hayo si maneno ya mtu mwengine bali ni maneno ya Asha Mohamed Ali  ambae anagombea Ubunge Jimbo la Wawi kwa tiketi ya Chama cha  United Democratic Party (UDP.) Mama huyo mwenye umri wa (45) mkaazi wa Wawi, wilaya ya Chakechake mkoa wa Kusini Pemba, ana watoto wanane (8),  wanawake watano na wanaume watatu, na  sasa yupo kwenye ndoa. Asha alizaliwa mwaka 1977 katika kijiji cha Mvumoni Wawi wilaya ya Chakechake mkoa wa Kusini Pemba, na elimu yake ni elimu ya msingi aliyoipata katika Skuli ya Sekondari  Ziwani. Asha  alianza safari yake ya kisiasa mwaka 2000, alivutwa na hamu ya kutetea haki za wananchi wa Pemba, hasa wanawake na vijana. Anasema msukumo wake mkubwa wa kujingiza kwenye harakati za kisiasa ulitokana na ushauri wa mume wake. Mume wake  aliemuoa mwanzo alikua kiongozi wa chama cha jahazi asilia, na yeye alimshauri na kujingiza kwen...

UMGOMBEA URAIS WA MUUNGANO WA UDP AAHIDI NEEMA LUKUKI KWA WAPEMBA

Image
  NA FATMA HAMAD, PEMBA MGOMBEA URAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Tiketi ya Chama cha United Demokratik Pati UDP Saum Hussein Rashid amesema endapo atachaguliwa na kupata ridhaa ya kuongoza atahakikisha anaboresha miundombinu ya afya, ili kuona huduma zote zinapatikana bure, ikiwemo huduma za mama na mtoto. Mgombea huyo aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi na wanachama wa chama hicho, katika mkutano uliofanyika Shamiani Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba. Alisema endapo atapata ridhaa na kuwa Rais wanchi atahakikisha  huduma zote za afya Hospitalini zinapatikana bure, hususani za mama na mto, ili kuepusha vifo vitokanavyo na uzazi. ‘’Nikiwa Rais nitahakikisha vifaavyote ambavyo vya kujifungulia  vinapatikana bure, mama awe amejifungua kwa uperashini ama kwa njia ya kawaida, zote tutazigharamikia sisi,’’alieleza. Aidha akitaja kipaumbele chengine atakuja na kilimo cha umwagiliaji, ambacho kitasaidia wananchi kupata chakula sambamba na kuzuia atahari za m...

WAFANYA BIASHARA TIBIRINZI WAMKABIDHI CHANGAMO ZAO MGOMBEA URAISI WA UDP

Image
  NA FATMA HAMAD, PEMBA WAFANYABIAshara wa soko la Tibirinzi Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba wamemtaka  Mgombea Urais  wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya chama cha United Demokratik Pati UDP, Saumu Hussein Rashid wakati atakapoingia madarakani kuwapunguzia Kodi. Wakizungumza na mgombea huyo baadhi ya wafanyabiashara hao akiwemo Kassim Kishuka, baada ya kuwatembelea katika biashara zao, walisema bei za vyakula ziko juu kutokana na ushuru mkubwa wanaotozwa, hivyo wamemtaka kulipa kipaumbele suala la kodi, ili bidhaa ziweze kushuka bei. ‘’Kwakweli bidhaa zimepanda bei mno, na hili ni kutokana na ushurumkubwa wa kodi, wafanyabiashara wenzetu wanashindwa kufanya  biashara, hivyo tunaomba suala la kodi uliangalie kwa hali ya juu pindi ukipata ridhaa ya kushika nafasi  hiyo. Walisema uchumi wa wananchi wa Pemba ni mdogo, hivyo endapo suala la kodi kama halitoangaliwa, bidhaa zitaendelea kupanda bei na kupatikana kwa mlo mmoja, jambo litalopelekea...

CHAMA CHA MAPINDUZI KUJA NA NEEMA KWA VIJANA NA FATMA HAMAD, PEMBA

Image
                    NA FATMA HAMAD, PEMBA CHAMA CHA Mapinduzi CCM Taifa kimesema moja ya vipaumbele vyake ni kutatua changamoto ya ajira kwa vijana, pindi wananchi watakapokichagua kushika madaraka na kuiongoza nchi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Mjumbe wa Halmashuari Kuu ya CCM Taifa Masoud Ali Mohamed alitoa kauli hiyo wakati akizungmza na wananchi na wanaccm katika Uzinduzi wa Kampeni za Jimbo la Tumbe pamoja na kuwanadi wagombea wa Ubunge, Uwakilishi na Udiwani, huko Viwanja Vya Gonga Mfupa Tumbe Mkoa wa Kaskazini Pemba . Alisema Chama Cha Mapinduzi kinafahamu Changamoto ya ajira Kwa Vijana, hivyo watakapokichagua tena kitaondosha Shida hiyo. ‘’Niwahakikishie vijana mtakapokichagua chama cha CCM naahidi nyote mtapata ajira, ambapo ndio shida yenu kubwa inayowaumiza,’’alisema. Alisema chamapekee ambacho kinaweza kuleta mabadiliko ni chama cha Mapinduzi, hivyo ni vyema mkakichagua tena, ili kije kiwe mkombozi wa ...