UMGOMBEA URAIS WA MUUNGANO WA UDP AAHIDI NEEMA LUKUKI KWA WAPEMBA


 



NA FATMA HAMAD, PEMBA

MGOMBEA URAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Tiketi ya Chama cha United Demokratik Pati UDP Saum Hussein Rashid amesema endapo atachaguliwa na kupata ridhaa ya kuongoza atahakikisha anaboresha miundombinu ya afya, ili kuona huduma zote zinapatikana bure, ikiwemo huduma za mama na mtoto.

Mgombea huyo aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi na wanachama wa chama hicho, katika mkutano uliofanyika Shamiani Chake chake Mkoa wa Kusini Pemba.

Alisema endapo atapata ridhaa na kuwa Rais wanchi atahakikisha  huduma zote za afya Hospitalini zinapatikana bure, hususani za mama na mto, ili kuepusha vifo vitokanavyo na uzazi.

‘’Nikiwa Rais nitahakikisha vifaavyote ambavyo vya kujifungulia  vinapatikana bure, mama awe amejifungua kwa uperashini ama kwa njia ya kawaida, zote tutazigharamikia sisi,’’alieleza.

Aidha akitaja kipaumbele chengine atakuja na kilimo cha umwagiliaji, ambacho kitasaidia wananchi kupata chakula sambamba na kuzuia atahari za mabadiiko tabianchi.

Alisema suala la mabadiliko ya tabia ni tatizo ambalo limekua likiathiri kwa kiasi kikubwa jamii, hivyo pindi akichaguliwa, ataanzisha kilimo cha umwagiliaji, wananchi wazalishe mazao na kupatikana chakula cha kutosha, sambamba na kujiepusha na athari zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati kuu Taifa UDP Erasto Nyaga Suzan alisema endapo Chama chao kitapata ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha analipa kipaombele suala la ajira, kuona vijana wote wanaajiriwa.

‘’Tutakapoingia madarakani tutahakikisha tunaweka miradi mbalimbali ambayo itawawezesha vijana kupata ajira kwa wingi,’’alisema.

Mapema Mjumbe wa Mkutani Mkuu wa Chama hicho Abass Mohamed Khatib aliwataka wananchi wa Chake chake kukiunga mkono chama chao, ili kije kiwaletee mabadiliko.

Nae mgombea Ubunge wa jimbo la Wawi, wa chama hicho Asha Mohamed Ali aliwataka wananchi kuendeleza mshikamano na umoja walio nao, na sio kubaguana kwa ajili ya siasa.

Alisema suala la siasa sio ugomvi wala chuki, hivyo ipo haja wananchi kushikamana kwa pamoja katika shughuli zote za kimaisha na wasibaguane kwa sababu ya vyama vyao.




Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO