CHAMA CHA MAPINDUZI KUJA NA NEEMA KWA VIJANA NA FATMA HAMAD, PEMBA


                    NA FATMA HAMAD, PEMBA

CHAMA CHA Mapinduzi CCM Taifa kimesema moja ya vipaumbele vyake ni kutatua changamoto ya ajira kwa vijana, pindi wananchi watakapokichagua kushika madaraka na kuiongoza nchi katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Mjumbe wa Halmashuari Kuu ya CCM Taifa Masoud Ali Mohamed alitoa kauli hiyo wakati akizungmza na wananchi na wanaccm katika Uzinduzi wa Kampeni za Jimbo la Tumbe pamoja na kuwanadi wagombea wa Ubunge, Uwakilishi na Udiwani, huko Viwanja Vya Gonga Mfupa Tumbe Mkoa wa Kaskazini Pemba .

Alisema Chama Cha Mapinduzi kinafahamu Changamoto ya ajira Kwa Vijana, hivyo watakapokichagua tena kitaondosha Shida hiyo.

‘’Niwahakikishie vijana mtakapokichagua chama cha CCM naahidi nyote mtapata ajira, ambapo ndio shida yenu kubwa inayowaumiza,’’alisema.

Alisema chamapekee ambacho kinaweza kuleta mabadiliko ni chama cha Mapinduzi, hivyo ni vyema mkakichagua tena, ili kije kiwe mkombozi wa   shida zenu.

Aidha alisema  kipaumbele Changine ni kudhibiti Mfumuko wa Bei za Bidhaa za Vyakula, kuona kila mwananchi anauwezo wa kula mlo uliotimia, ili kuwa na jamii yenye afya bora.

Alisema moja ya eneo ambalo serikali ya Mapinduzi imeweka kipaumbele ni kupunguza kodi za vyakula, ili wananchi waondokane na njaa, na wajasiriamali wamudu kufanya biashara.

Sambamba na hilo alisema wataweka ghala la kuhifadhia bidhaa, kuona vyakula vinapatikana kwa muda wote na bila kupanda kwa bei, hatakama duniani kimepungua.

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumujiya ya Wazazi Mkoa wa Kaskazini Pemba Ramadhan  Issa Kipaya na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Micheweni Ali Masod Kombo wamewataka wananchi wa Jimbo la Tumbe kutofanya makosa kwa kuwachagua Viongizi makini, ambao wanaweza kusimama na kutetea kero zao.

Walisema wakati umepita wa kuchagua kiongozi kwa sababu ya chama Fulani ama kwa kipato chake, wachague watu ambao wanauzalendo nan chi yao na wananchiwao.

Naye Mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Tumbe Salma Khamis Tumu alisema atakapochagualiwa na wananchi na kuwa mwakilishi wa Jimbo hilo ataelekeza nguvu zake katika kuinua Vikundi Vya Ushirika kwa kuvipatia usajili na Mitaji.

‘’Naamini katika jimbo langu kuna vikundi vingi vya ujasiriamali lakini havifikii malengo yao kutoana na kukosa mitaji, hivyo mkinipa kura za ndio nitahakikisha naviimarisha kwa kuvipatia mitaji viweze kuzalisha bidhaa kwa wingi na zenye ubora,’’alisema.

Aidha kwa upande mwengine alisema atahakikisha anapigania maslahi ya watu wenyeulemavu, ili kuona nawao hawaachwi nyuma katika fursa mbali mbali za kimaendeleo ambazo zinakuja katika jimbo lake.

‘’Nitakapokua muwakilishi sitokubali kuona mtu mwenye ulemavu amefungiwa ndani, nitapambana kila mtoto mwenye ulemavu anapata haki zake stahiki iwe ya elimu, afya sambamba na kushiriki katika miradi yote ya maendeleo ambayo imekua ikitokezea shehiani mwao,’’alisema.

 
Maryam Hemed na kutoka Jimbo la Tumbe waliahidi kumuunga mkono mwakilishi wa jimbo hilo, kwa vile ni mwanamke mwenzao, ili aje asimame na kutetea shida za wanawake wenzake.

Walisema shida za wanawake anazijua mwanamke vile vile, hivyo walisema watahakikisha  wanampa kura za ndio, jami ya wanawake ije iwe rahisi kumfika na kumuelekezea matatizo yao.

 Walisema mgombea huyo alishakamata nafasi ya udiwani miaka iliyopita na kuna mengi mazuri aliyowafanyia, hivyo wataendelea tena kumrudisha kwenye maamuzi, akasimame ni kuzisemea kadhia za watu wa Tumbe.



 


 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO