ASHA MOH’D ALI MWANAMKE MWENYE NDOTO YA MABADILIKO
NA MOZA SHAABAN,PEMBA
NATAMANI moja niwe kiongozi nilete mabadiliko katika Jimbo langu.
Hayo si
maneno ya mtu mwengine bali ni maneno ya Asha Mohamed Ali ambae anagombea Ubunge Jimbo la Wawi kwa tiketi
ya Chama cha United Democratic Party
(UDP.)
Mama huyo mwenye umri wa (45) mkaazi wa Wawi, wilaya ya
Chakechake mkoa wa Kusini Pemba, ana watoto wanane (8), wanawake watano na wanaume watatu, na sasa yupo kwenye ndoa.
Asha alizaliwa mwaka 1977 katika kijiji cha Mvumoni Wawi
wilaya ya Chakechake mkoa wa Kusini Pemba, na elimu yake ni elimu ya msingi
aliyoipata katika Skuli ya Sekondari
Ziwani.
Asha alianza safari
yake ya kisiasa mwaka 2000, alivutwa na hamu ya kutetea haki za wananchi wa
Pemba, hasa wanawake na vijana.
Anasema msukumo wake mkubwa wa kujingiza kwenye harakati za
kisiasa ulitokana na ushauri wa mume wake.
Mume wake aliemuoa
mwanzo alikua kiongozi wa chama cha jahazi asilia, na yeye alimshauri na
kujingiza kwenye harakati za kisiasa kupitia chama cha UDP.
‘’Kwa kusema kweli mimi hizi harakati nimerithi kwa marehemu
mume wangu, mungu amuweke pahali pema sito msahau kwani yeye ndie alienifikisha
hapa nilipo sasa,’’anaeleza.
USHIRIKI
WAKE KWENYE CHAGUZI
Asha si mgeni kwenye siasa
za ushindani, alishawahi kugombea mara (3), na hii ni mara ya nne
kugombea ubunge jimbo hilo hilo la Wawi.
‘’Nilishagombea mara tatu sijafanikiwa, sijakata tamaa na
kwa uwezo wa Mungu marahii ninaimani kubwa nitafanikiwa kulikamata jimbo, ili
niwaletee wanawawi maendeleo,’’anasema.
Anasema safari yake imekua na changamoto, lakini pia
anamafanikio ya kujenga mtandao mpana kwa wafuasi wake.
Anaeleza kuwa alishawahi kushika nafasi ya Katibu wa akinama
Taifa kwa muda wa mika mitano, na sasa ni mjumbe wa bodi ya wadhamini, katika
chama chake.
Awali anaingia sasa kwenye mchakato huo wa kinyanganyiro cha kugombea familia yake ilikua
haimpi mashirikiano, ilikua wanahisi wakimchagua kama wanazitupa kura zao.
‘’Mwanzoni mwa mwaka 2000, wakati naanza sasa hata familia
yangu ilikua haikopamoja na mimi kura zao walikua wazipeleka kwa Chama cha CUF
ambapo kwa sasa ni ACT Wazalendo,’’anasema.
Ingawa kuanzia Uchaguzi uliopita wa 2020, walibadilika na
walinipa kura zao na nilipata kuranyingi, na hadi sasa wakobega kwa bega na
mimi kwa kila hatua ninayopitia.
SERA
ZAKE KUU
Sera zake ambazo anazizungumzia katika kampeni zake ni
kuwapatia wanavikundi miundombinu ya kisasa ya kilimo, kuwatafutia mbegu bora pamoj na mitaji,
wazalishe mazao ya biashara na ya chakula, kupatikane chakula cha kutosha na
kuondokana na janga la njaa.
Sambamba na hayo anasema endapo atachaguliwa atahakikisha
anawangalia walimu wa Madrasa za Qur an kwa kuwapa mshahara.
‘’Walimu wa Madrasa wengi ni masikini, naahidi nitakapokua
mbunge nitahakikisha walimu wa madrasa nawapa mshahara walimu wa madras kama
walimu wengine, ili waendeleze kitabu cha mwenyezi Mungu,’’anaeleza.
Mama huyo anasema ni wakati kwa jamii kuwachagua viongozi wanawake
katika majimbo yao, wawaletee maendeleo.
MSAADA WA FAMILIA YAKE
Familia ya Asha imekua msaada mkubwa katika safari yake
hiyo,kwani wamekua wakimsaidia kifedha, kimaombi na hata kushiriki katika
mikutano yake ya kampeni anayoifanya, na ile ya kuenda nyumba kwa nyumba.
‘’Pesa ambazo nilikwenda kuchukulia fomu nilidundulikiza
kwenye biashara zangu, na nyengine nilipewa na familia yangu” anasema.
Kutokana na mshikamano huo ambao amekua akiupata kupitia
kwa familia yake, umekua moja ya nguzo
ya kuimarisha nafasi yake kisiasa, na inamfanya kuwa na matumaini makubwa ya
kufikia ndoto zake za kuwa kiongozi.
MUME
WAKE
Anasema alipomuoa alimkuta na harakati zake hizo za kisiasa
hajawahi kumzuia hata siku moja kufanya shughuli zake hizo.
Anasema amekua akimsaidia kwa kila hatua iwe nikwa pesa ama
kwa ushauri, ili aweze kufanikiwa katika harakati zake hizo.
‘’Sijafanya wivu wala sijamkataza nimekua nikimsaidia kwa
kila hatua, afanikiwe naamini akipata ataisaidia familia yetu, na hata wanawake
wenzakeambao wanamzunguka,’’anaeleza .
Anasema kwa vile mke wake huyo ni mtu anaependa maendeleo na
amekua ni mwenye kujali, endapo atapata nafasi ataondosha kero zinazowakwaza
wananchi, ili waishi kwa matumaini.
‘’Naamini ipo siku atafanikiwa kwani nimtu ambae hapendi
kukata tama, na mtu mwenye kujiamini na mwenye kujitambua.
MTOTO WAKE
Omar Saleh Khalfan ni
mtoto wa mama huyo anasema tokea alipofahamu mama yake yupo katika harakati za
kisiasa, amekua akigombea nafasi ingawa hajawahi kushika jimbo.
Anasema suala la uongozi kwa mwanamke ni jambo zuri, hivyo
kitendo anachokifanya mama yao sio kitendo kibaya kwani, kinaweza kuja kuleta
mabadiliko katika familia yao na hata kwa wananchi wa jimbo lao.
‘’Nimekua nikimsaidia mamayangu kwa kila hatua, aweze
kufanikiwa, na namini siku moja atakuja kuwa mtetezi wa wanyonge hasa wanawake
na watoto,’’anasema.
Anasema mtoto hufuata kichogo cha mlezi wake kwani nayeye
amekua ni mwanasiasa mkubwa katika Chama hicho cha UDP.
KIONGOZI
WA CHAMA CHAKE
Juma Khamis Faki Naibu Ktibu mkuu wa Chama cha UDP anasema Asha ni mwanamke jasiri, muaminifu
na mwenye kupenda maendeleo ya wenzake.
Anaamini endapo atapata ridha ya kuwa Mbunge maendeleo ya
wananjimbo la wawi yatapatikana na shida zinazowakabili atazisimamia vyema na kuzitetea.
‘’Asha ni mwanamke mpambanaji anapenda mashirikiano na
wenzake, endapo kama atapita naamini jimbo la Wawi litan’gara kwa
maendeleo,’’anasema.
Anasema kutokana na mafunzo mbali mbali ya uongozi ambayo
wamekuwa wakiwapatia wanawake wa Chama chao yameweza kumjenga na amekua na
uthubutu na shauku ya kutaka kua kiongozi, alete mabadiliko ndani ya jimbo
lake.
WANAHARAKATI
Chama cha Wandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA
Zanzibar kimekua kikiwaelimisha wanawake juu ya masuala ya uongozi,
wajitokeze kwa wingi kwenye mchakato wa Uchaguzi
na kuwania nafasi majimboni, kwani ni haki yao kikatiba.
Amina Ahmed Mohamed Mratibu kutoka TAMWA Pemba anasema lengo
la kuwaelimisha wanawake hao ni kuwa na uthubutu wa kugombea nafasiza uongozi,
ili watatue kero za wanawake wenzao katika majimbo yao pindi wakipata
nafasihizo.
‘’Shida za wanawake anazijua mwanamke, na ndio maana tunawahamasisha
wagombee waende wakatatue hizo shida za wanawake wenzao,’’anasema.
Hii ni ishaza nzuri ya mabadiliko, huku Asha Mohammed Ali
akiwa miongoni mwa wanawake wanaothubutu kushindana moja kwa moja kwenye
majimbo badala ya kutegemea viti maalumu.
TAKWIMU
Kwa mujibu wa Chama cha Wandishi wa Habari WAnawake Tanzania
Tamwa Zanzibar kupitia ripoti iliyotolewa na Tume ya Uchaguzi Zanziba mwaka
2020, kupitia nafasi ya Uwakilishi kwenye majimbo 50 ya Zanzibar wanawake
waliojitokeza ni 61 walioshinda ni 8 na wabunge wanawake waliowakilisha Zanziba
ni wane.
Takwimu kutoka Tume huru ya Uchaguzi Tanzania kwa upande wa
wabunge walikua 141 walioshinda wanawake ni wane tu.
Kwa Uchaguzi wa mwaka huu 2025, unaweka historia mpya, kwani
ni mara ya kwanza wanawake kujitokeza kwa wingi
kuwania nafasi mbalimbali ikiwemo Urais, Ubunge, Uwakilishi
na Udiwani.
Kwa vile suasa la uchaguzi ni haki ya kila mtu kama katiba Katiba
yetu mama ya nchi ya mwaka 1984 inavyoeleza katika kifungu cha 21,(2) kinaeleza
mzanzibari yoyote anahaki na uhuru wa kushiriki kikamilifu katika kufikia maamuzijuu
ya mambo yanayo muhusu yeye, maisha yake au yanayohusu Taifa lake.
Hata Mikataba ya kimataifa ya haki za kiraia na haki za
kisiasa ya mwaka 1966 kifungu cha 25, kila raia ana haki ya kupiga kura na
kuchaguliwa katika uchaguzi wa kweli, wa haki na wa mara kwa mara, uliofanywa
kwa kura ya siri na kuhakikisha uhuru wa wapiga kura.
Comments
Post a Comment