WAFANYA BIASHARA TIBIRINZI WAMKABIDHI CHANGAMO ZAO MGOMBEA URAISI WA UDP
Wakizungumza
na mgombea huyo baadhi ya wafanyabiashara hao akiwemo Kassim Kishuka, baada ya
kuwatembelea katika biashara zao, walisema bei za vyakula ziko juu kutokana na
ushuru mkubwa wanaotozwa, hivyo wamemtaka kulipa kipaumbele suala la kodi, ili
bidhaa ziweze kushuka bei.
‘’Kwakweli
bidhaa zimepanda bei mno, na hili ni kutokana na ushurumkubwa wa kodi,
wafanyabiashara wenzetu wanashindwa kufanya biashara, hivyo tunaomba suala la kodi
uliangalie kwa hali ya juu pindi ukipata ridhaa ya kushika nafasi hiyo.
Walisema
uchumi wa wananchi wa Pemba ni mdogo, hivyo endapo suala la kodi kama
halitoangaliwa, bidhaa zitaendelea kupanda bei na kupatikana kwa mlo mmoja,
jambo litalopelekea tatizo la udumavu kwa wakaazi wa kisiwa hicho.
Aidha kwa
upande wao Mohammed Juma Rehan na Omar Mgando
wamemtaka mgombea huyo kuhakikisha anawajengea soko la kisasa na lenye hadhi,
ili wapate sehemu salama ya kufanyia biashara zao.
Walisema
wamekua wakilipa kodi, lakini eneyo ambalo wanakaa na kufanyia biashara zao sio
rafiki, kwani hata inaponyesha mvuainabidi wahame na kutafuta pahala pengine pa
kujificha.
‘’Bado
hatujakua na soko, unaona hapa tupo uwanjani na samaki wetu, sio mazingira
rafiki kwetu, jee ikitokezea mvua unafkiri tunahangaika kiasi gani, tunaambiwa
tukaingia ndani ya soko juu jee samaki tutauzaje uko juu gorofani, walisema.
Sambamba na
hilo walisema wanahitaji kujengewa soko kubwa na lenye hadhi, wafanyabiashara
wa aina zote wauze bidhaa zao humo, ili kuona bidhaa zote zinapatikana.
‘’Tutakapopata
soko kubwa na kila bidhaa ikawepo hapa, wananchi watanunua vitu vyote humu, na
sio nazi anunue hapa, samaki akanunue machomane,’’hiyo ni shida.
‘’Toka
kampeni zilipoanza hatujawahi kumuona mgombea yoyote kuja na kutusikiliza shida
zetu, wewe ndo wa mwanzo hivyo tunahakikisha tunakunga mkono wewe mwanamke
kwani ulishaonesha mwelekeo mzuri kwetu,’’alisema.
Nae Mgombea
huyo wa Urais Saum Hussein Rashid alisema lengo la kuwatembelea wajasiriamali
hao ni kusikiliza changamoto ambazo zimekua zimekuwa zikiwakabili, aweze
kuzifahamu, ili aje kuzitatua pindi akipata ridhaa.
Alisema sera
ya Chama chao ni kuwainua wanchi kiuchumi, hivyo watahakikisha wanazitatua kero
zinazowakwaza, ikiwemo kodi, na kuwapatia mitaji, waendeleze biashara zao,
waweze kukuza kipato chao.
‘’Sisi sera
yetu ni kuinua kipato cha wananchi, hivyo tutahakikisha kodi imepungua, na
tutawapa mitaji wafanyabiashara waendeleze biashara zao, na wajiinue kiuchumi
na kuondokana na umaskini,’’alieleza.
Aidha
alisema kipaumbele chengine ni kuweka kiwanda kikubwa cha usindikaji wa Samaki,
kuona soko linaimarika ndani na nje ya nchi, sambamba na kupatikana kwa
kitoeleo cha kutosha.
Mgombea huyo
aliwasili kisiwani Pemba leo asubuhi, ambapo mbali ya kuwatembelea
wajasiriamali hao alitembelea kaburi la aliekuwa Makamo wa Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dokta Omar Ali Juma, na kuifariji familia yake.



Comments
Post a Comment