Wananchi wahimizwa kujiandikisha kwenye daftari la mpiga kura
NA FATMA HAMAD PEMBA. Wananchi ambao wameshafikia sifa za kuwa wapiga kura wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura linalotarajiwa kuanza hivi karibuni. Wito huo umetolewa na Makamo mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstafu wa Mahkama ya Rufaa Mbarouk Salim Mbarouk katika mkutano wa wadau wa Uchaguzi kuhusu uboreshwaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura, huko Makonyo Chake chake Pemba. Amesema ili kufanikisha ipasavyo zoezi hilo ni vyema wananchi kushirikiana na tume huru ya uchaguzi,na kuhakikisha wenye sifa za kuwa wapiga kura wanajitokeza kujiorodhesha kwenye daftari hilo. ‘’Ndugu wananchi tufahamu Tume huru ya uchaguzi imeanza na zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la mpiga kura,hivyo tuhakikishe kila mwenye sifa anapata haki yake hiyo,’’alisema. Alisema kwa mujibu wa kifungu cha...