Wanafunzi wapewa mbinu ya kujikinga na udhalilishaji
Hayo
yamesemwa na Msaidizi wa Sheria shehia ya Tumbe mashariki wakati akizungumza na
wanafunzi wa Skuli ya Shumba vyamboni katika mkutano malummu ulioandaliwa na
Jumuia ya wasaidizi wa sheria wilaya ya Micheweni Pemba.
Alisema
vitendo vya udhalilishaji hufanyika kila sehemu ikiwemo Madrasa,
Skuli,Majumbani,hivyo ni budi kutoa tarifa wakati watakapofanyiwa.
‘’Msiyafiche
matendo ya udhalilishaji hata kama mmefanyiwa na watu wenu wa karibu akiwemo
mwalimu,kaka Mjomba toeni tarifa msione aibu’’,alisema.
Mapema
msaidizi wa sheria shehia ya Tumbe Mashariki Fatma Hamad Faki aliwasisitiza
wanafunzi hao wasipoke zawadi ya aina yoyote wanazopewa na watu ambao si wazazi
wao ili kujikinga na vitendo vya udhalilishaji.
‘’Niwaombe
ndugu zangu msishawishike na wala msipoke vizawadi mnavyopewa na watu ambao si
maharimu zenu ni hatari
jiepusheni’’,aliwasisitiza.
Kwa upande wake Said Salim Khamis msaidizi wa sheria shehia ya Msuka aliwanasihi wanafunzi hao kushughulikia masomo yao kwanza ili waweze kufikia ndoto zao za badae.
Nae mwalimu anaeshughulikia kambi ya wanafunzi hao Seif Khamis amewashukuru watendaji wasaidizi wa sheria hao kwa kufika katika Skuli yao na kuwapatia elimu hiyo ya masuala ya udhalilishaji kwani inaweza ikawa dawa na kuogopa kufanya vitendo hivyo.
Comments
Post a Comment