Wizi wa Simu wamsababishia kwenda Jela miezi 6.

 
 

 


                              NA FATMA HAMAD,PEMBA

Msifunzwa ni babae hufunzwa ni ulimwengu usemi huu umemkuta Sudi Hamad Salim mwenye umri wa mia 26 mkaazi wa Jadida Wete Pemba, kwenda Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miezi Sita baada ya kukubali kosa lake siku ya mwanzo ya kusomewa kesi yake.

Awali mshtakiwa huyo akisomewa shauri lake  katika  Mahkama ya Wilaya iliyopo Wete  na Mwendesha mashtaka wa Serikali kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Juma Mussa Omar  alikiri kosa lake la kuiba Simu aina ya Tecno Spark  8 yenye thamani ya shilingi Laki 400,000 /=.

 Mwendesha mashtaka huyo wa Serikali aliiambia Mahkama hiyo ya wilaya kwamba kwa vile mshtakiwa huyo amekiri kosa lake mwenyewe, ni vyema  kupewa adhabu kali ili iwe somo kwake na kwa wengine.

 ‘’Mheshimiwa Hakimu kwa vile mshitakiwa amekubali kosa lake mwenyewe, hivyo, tunaomba itolewe adhabu kali kwani itakuwa ni fundisho kwake,alieleza DPP’’.

Hakimu wa Mahkama hiyo Maulid Hamad Ali alieleza kuwa kwa vile mshitakiwa hakuisumbua Mahkama amekubali kosa mwenyewe bila kulazimishwa atatumikia Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miezi Sita au alipe Faini ya shilingi Laki 300,000.

Mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo  Mei 13 mwak huu saa 12:30 za jioni huko Jadida Wete aliiba Simu aina ya Tecno Spark 8 yenye thamani ya Shilingi Laki 400,000 mali ya Nasra Ali Bakar, jambo ambalo ni kosa kinyume na kufungu cha 251 (1) na 258 cha Sheria ya Adhabu, Sheria namabari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.


Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO