SIMU YAMPELEKEA KWENDA JELA MIAKA MINNE

 
Mama wa miaka 58 afungwa jela miaka 29 kwa kumbaka mvulana wa miaka 8

 

                              NA FATMA HAMAD,PEMBA

HAKIMU wa Mahkama ya Mkoa  Wete Zuwena Mohamed Abdulkadir  amemuhukumu kwenda chuo cha mafunzo kwa kipindi cha miaka minne   Ali Mbarouk  Suleiman mwenye  (18) mkaazi wa Konde Chanjaani  baada ya kutiwa hatiani kwa kuvunja Nymba usiku na kuiba  Simu.

Mshitakiwa huyo ametiwa hatiani kwa makosa ya kuvunja nyumba na kuiba Simu moja aina ya Sumsung  yenye thamani ya shilingi 138,000/=, kwa makisio mali ya  Said Mohamed Salim .

Aidha Hakimu huyo alieleza kuwa kosa la kwanza la kuvunja Nyumba usiku atatumikia  chuo cha mafunzo kwa muda wa mika mitatu, na kosa la pili la kuiba Simu atumikie kwa muda wa mwaka mmoja.

Mbali na adhabu hiyo pia alitoa agizo la kurejeshwa simu kwa mwenyewe mmiliki wa simu hiyo ambayo ilikua ni kielelezo cha ushahidi Mahkamani hapo.

 Mwendesha mashtaka wa serikali Mohamed Ali Juma alieleza kuwa kwa vile Mahkama imemuona na hatia mshitakiwa huyo ni vyema kutoa adhabu kali kwa kijana huyo.

Aliendelea kusema kuwa masuala ya wizi hususani usiku ni masuala ambayo imekua ikisumbua jamii, hivyo isimuonee huruma impe aghabu kama sharia inavyoelekeza.

‘’Mheshimiwa tunakuomba kwamba umpe adhabu kali kama sharia ilivyo elekeza, kwani wizi ni masuala ambayo imekuwa ni kero kwa jamii na hata Taifa,alisema’’

Baada ya maelezo hayo ya mwendesha mashataka ndipo alipomwamuru kutumikia Chuo cha Mafunzo kwa muda wa miaka mine.

Mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Februari 20 mwaka huu, majira ya saa tatu na saa nne usiku  katika Kijiji cha Chanjaani Konde  alivunja nyumba ikiwa kosa kifungu cha 290 (1) na 291(`1) ( a) ( 2) cha Sheria ya Adhabu sharia nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.

Kosa la pili kuiba Simu moja aina ya SUMSUNG yenye thamani ya shilingi 138,000/=kwa makisio, ambapo kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 251( 1) na 258 vya sharia nambari 6 ya mwaka 2018 sheria ya Zanzibar.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO