wanafunzi wametakiwa kujiepusha na vigenge viovu





 

                       NA FATMA HAMAD,PEMBA

Wanafunzi maskulini wametakiwa kujiepusha na vitendo hatarishi ambavyo vitasababishwa kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao.

Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria wilaya ya Micheweni (MIDIPAO)Hemed Said Masoud wakati akizungumza na wanafunzi wa Skuli ya Tumbe Sekondari alisema kuwa wapo baadhi ya wanafunzi wamekua wakijingiza katika magenge maovu ikiwemo Ubakaji,wizi na ulevi.

Alisema elimu ndio mkombozi mkubwa wa maisha, hivyo ni vyema wanafunzi kutumia muda wao kwa kujipatia elimu ambayo itakuja kuwaletea manufaa kwao na hata kwa familia zao.

‘’Niwausie wananfunzi wangu muda ukipita haurudi tena, hivyo itumieni fursa mlionayo kwa ajili ya kujipatia elimu bora ili isije ikawa majuto kwenu ya hapo badae,alisema mkurugenzi.’’

 Mapema msaidizi wa Sheria shehiya Tumbe Magharibi Suleiman Hemed aliwataka wanafunzi hao kutoa tarifa kwa watu wao wa karibu wakati watakapoona vitendo vinavyoashiria utovu wa nidhamu katika maeneo yao yanayowazunguka.

‘’Udhalilishaji unaweza ukafanyika kila pahala, hivyo musifiche semeni kwa watu wenu wa karibu,ili muepukane na vitendo hivyo,alieleza’’

Nae Riziki Ali Hamad Msaidizi wa sheria kutoka shehia ya Chamboni Micheweni aliwataka wanafunzi hao kuvaa nguo ambazo ambazo hazioneshi maungo yao, jambo ambalo litawaepusha kufanyiwaudhalilishaji.

‘’Wanafunzi msipovaa nguo wakati mnapokuja Skuli mnaweza kuwashawishi wahalifu kuwafanyia vitendo viovu,alisema’’


 

 

 

 

 

Comments

Popular posts from this blog

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

‘’KATIBU MKUU ELIMU ‘’TOENI ELIMU YA MALEZI BORA’’

UROHO WA MALI KWA WANAUME UNAVYONYIMA WANAWAKE ARDHI