Wakulima waikumbusha jambo Serikali


NA FATMA HAMAD, PEMBA

Wananchi kisiwani Pemba ambao walikatiwa mikarafuu yao kwa ajili ya kupisha miundombinu ya umeme wameiomba Serikali ya Mapinduzi kuwalipa fidia zao wakulima hao.

Wakizungumza katika hafla ya ugawaji wa zawadi kwa washindi wa Vuna na Tigo pesa mkulima Khamis Juma Khamis na Halima Mohamed Seif huko Makonyo Chake chake Pemba walisema walikatiwa mikarafuu yao na kuahidiwa kulipya ila hadi leo hakuna chochote walichokipata.

Walisema kuwa karafuu ndio zao kuu wanalolitegemea kujipatia kipato, hivyo ni vyema Serikali kulikalia kitako na kuhakikisha wanalipatia ufumbuzi suala hilo.

‘’Tulikatiwa Mikarafuu yetu na tukaahidiwa tutalipwa ila hadi sasa hakuna lolote tulilolipata’’,walisema.

Mapema mkulima Ali Kombo Hamad alisema katika msimu wa karafuu ujao ni vyema shirika la biashara la ZSTC kuboresha miundombinu ya kiwanda cha kununulia Makonyo kilichopo wawi, kuhakikisha kinafanya kazi ili kuwaondoshea usumbufu wananchi wanao kuja kuuza makonyo yao.

‘’Tulichukuliwa viwanja vyetu kwa ajili ya kujengewa kiwanda cha kuzalishia Mafuta ya Makonyo ila tunaona hakina faida yoyote, tunahangaika,’’pakuzia makonyo yetu,’’alisema.

Kwa upande wake Ali Juma Ali alilitaka shirika la Biashara la ZSTC kuhakikisha wanapogawa Mikarafuu kwa wakulima kuwapatia miche ya kutosha ambayo itawafanya waweze kuotesha na kuzalisha kwa wingi.

‘’Unaweza ukapanda mashina 15 ikaweza kuota  mitatu, hivyo tunaomba mnapotoa msitupe miche kidogo,’’alidai


Nae waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Omar Said Shaban aliwatoa hofu  wakulima hao huku akiwahidi kulipwa fidia zao ndani ya mwaka huu wa 2024.



  

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO