Posts

Showing posts from September, 2025

Naibu Chauma asema: ‘’Chagueni viongozi wenye imani na Nchi yao’’

Image
  NA FATMA HAMAD, PEMBA Wananchi wametakiwa  kuwachagua  viongozi  ambao  wanauthubu na wenye uzalendo na nchi yao, wanaoweza kusimama na kutetea shida zinazowakwaza wananchi wao. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma Chauma Zanzibar, Mohamed Masoud Rashid  wakati akizungumza na wanachama na wananchi wa chama cha Chauma, katika uzinduzi wa kampeni za wagombea wa Ubunge, Uwakilishi na Udiwani huko Tumbe wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba. Alisema wakati umepita wa kuchagua viongozi kwa ajili ya chama ama kwa cheo chake, bali ni vyema kuhakikisha wanawachagua ambao wanauchungu na nchi yao na wanauwezo wa kutetea kero za wananchi, sambamba na kuwaletea mabadiliko. ‘’Nduguzangu wanatumbe badilikeni msichague viongozi ambao hawana maendeleo, isiwe wanaishia kupiga kofi tu kwenye meza,’’alisema. Aidha alisema endapo chama chao kitaingia madarakani, jambo la kwanza watakalolifanya ni kushusha bei za vyakula, ili kuona kila mwananc...

Wajasiriamali walia na uhaba wa malighafi za kusarifia bidhaa.

Image
    NA FATMA HAMAD,PEMBA WANAWAKE WAJAsiriamali kisiwani Pemba wamelalamikia juu ya kukosa sehemu maalumu ya kununulia malighafi kwa ajili ya kutengenezea bidhaa  kama vile, Crab pamoja na sabuni. Wajasiriamali hao wametoa kauli hiyo wakati wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumaliza mafunzo maalumu ya utengenezaji wa bidhaa za vyakula kama vile Makwaru na Achari, huko Ofisi za Jumuiya ya Uhifadhi wa Misitu CFP, Minyenyeni Wete Kaskazini Pemba.  Maryam Mbarouk Khamis mjasiriamali kutoka Kambini Mchangamdogo na Aisha Ali Hamad wa kiuyu minungwini walisema wamekua wakipata mafunzo kadhaa,  lakini wanashindwa kuzalisha kutokana na kukosa mali ghafi kwa ajili ya kutengenezea bidhaa hizo. ‘’Tunataka vitu tutengeneze lakini sehemu ya kununua ivo vifaa vya kutenezea bidhaa kama vile Ckirabu, shampuu, sabuni hapana, mpaka tuagizishie nje ya Pemba, hilo sisi wajasiriamali wachanga linatukwaza,’’walisema. Walisema  kwa vile serikali ya a...

WANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUEPUKA HABARI ZA UDANGANYIFU

Image
NA FATMA HAMAD, PEMBA WAANDISHI wa habari wametakiwa kufuata maadili wakati wanapotekeleza majukumu yao sambamba na kuandika habari zenye ukweli, zenye kulinda haki, heshima na utu wa binadamu, hasa katika kipinidi hiki cha kuelekea Uchaguzi mkuu wa Octoba mwakahuu. Wito huo umetolewa na Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu Zanzibar Khatib Mwinchande wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu, uzingatiwaji wa haki za Binadamu na Misingi ya Utawala bora katika mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2025, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ofisi hiyo Chake Chake Kusini Pemba. Alisema, ni vyema waandishi wa habari kufuata miiko na maadili yao wakati wanapotekeleza kazi zao, hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu wa Octoba 2025. Alifafanua, waandishi wa habari ni wadau muhimu wanaopaswa kuzingatia utekelezaji wa Sheria, kwani kufanya hivyo kutawasaidia kufanyakazi za ukweli, zenye kulinda haki na utu wa binadamu. Alisema, suala la uchaguzi ni mchakato muhimu katika Nchi, in...

WWAANDISHI WA HABARI WAOMBA KUPATIWA TAARIFA SAHIHI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025

Image
                               Zanzibar- Sept 28, 2025 Siku ya haki ya kujua duniani ni siku muhimu hasusan katika kuimarisha ufahamu wa wananchi na waandishi wa habari kama nguzo kuu za kuimarisha demokrasia, utawala bora na uwajibikaji ambapo ni vigezo muhimu katika kuleta maendeleo ya nchi.   Ufanisi wa wananchi na haki yao ya msingi ya kuweza kufahamu na kujua masuala mbali mbali ambayo yataweza kuimarisha maisha yao na kuwa na maendeleo katika jamii na taifa kwa ujumla.   Siku ya hii kujua huadhimishwa kila mwaka ifikapo tarehe 28 Septemba, kwa lengo la kukuza uelewa kwa wananchi na hata waandishi wa habari juu ya haki hii, kwani imekuwa ni changamoto kupata taarifa muhimu pale wananchi au waandishi wa habari wanapohoji masuala mbalimbali ya shughuli za serikali au taasisi za binafsi.   Katika maadhimisho haya, tunapenda kuangazia umuhimu wa haki hii kama chombo cha kuimarisha dem...

Serikali kujenga uwanja wa ndege wa kisasa Pemba

Image
NA FATMA HAMAD, PEMBA Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Awamu ya Nane imedhamiria kufanya mageuzi  makubwa katika sekta ya Usafiri wa Anga Zanzibar, kwa lengo la kuimarisha miundombinu ya utoaji wa huduma katika uwanja wa ndege wa Pemba pamoja na kuifungua Pemba Kimataifa. Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hussein Ali Mwinyi katika uzinduzi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba na Barabara ya Mkoani Chake Chake uliofanyika Viwanja vya uwanja wa Ndege Pemba.   Alisema ujenzi wa miradi hio ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM  ya mwaka 2025 ambapo malengo ya serikali ni kuhakikisha kuwa Pemba inakuwa na Uwanja wa ndege wa Kimataifa ambao utaifungua Pemba kwa kukuza utalii, uwekezaji na biashara.    Alisema   kuwa  serikali imejipanga katika kuhakikisha barabara zote za Zanzibar zinajengwa kwa kiwango cha lami na kuwa katika hali n...

Mgombea Urais ADC Aahidi kupunguza kodi wakati akiingia madarakani.

Image
              NA FATMA HAMAD,PEMBA MGOMBEA Urais Zanziba kwa tiketi ya Chama cha Allance for Democratic Change ADC Hamad Rashid Muhamed amesema endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi na kuwa Rais, atahakikisha anapunguza mtiririko wa kodi, ili kupunguza bei za bidhaa na kila mwananchi amudu kununua. Mgombea huyo ameyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi pamoja na wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni uliofanyika Micheweni Kaskazini Pemba. Alisema   ushuru   wa bidha umekua mkubwa, na kupelekea bidhaa kupanda bei, hali inayowakosesha baadhi ya wananchi wenye kipato cha chini kushindwa kupata chakula cha uhakika. ‘’Nitakapo kua Rais nitahakikisha napunguza asilimia 10 ya kodi, na kila mfanyabiashara atakua na tin namba yake ya kulipa, ili kupunuza mtiririko na ubadhilifu,   na   mapato   yaingie serikali moja kwa moja,’’alieleza. Aidha kwa upande mwengine Mgombea huyo alisema atahakikisha analibor...

‘’KIMBILIENI HOSPITALI NA SIO KWA WAGANGA MNAPOONA DALILI ZA TB’’

Image
NA FATMA HAMAD, PEMBA WANANCHI wamehimizwa kujitokeza Hospitali   kupima afya zao wakati wanapojihisi na dalili za ugonwa wa Kifua kiku,ili waweze kugundulika na kupatiwa tiba mapema, na sio kukimbilia kwa waganga wa jadi. Kauli hiyo imetolewa na Afisa Habari Tehama na Mawasiliano kutoka Kitengo shirikishi Ukimwi, Homa ya Ini, Kifua kikuu, na Ukoma Khalifan Khamis Khalifan wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi huko Ofisini kwake Chak chake mkoa wa Kusini Pemba. Alisema kwa mujibu wa utafiti wa Shirika la Afya Duniani (WHO)  unaonesha kwamba ugonjwa wa kifua kikuu upo, ingawa bado wagonjwa kugundulika ni shida. Alisema  takribani asilimia 80 ya wagonjwa kuwagundua inapotea, na hubakia katika jamii  na kutumia dawa za waganga wa jadi. ‘’Licha ya jitihada mbalimbali zinazofanyika kuondosha ugonjwa huo, bado watu hawaji Hospitali, wanaendelea kwenda kwa waganga wa jadi kwani wanaimani kwamba wamerogwa,’’alisema. Alisema wananchi waliowengi wanaamini kwamba ...

Wanawake wanaolima kilimo msitu Mchanga mdogo walia kukosa ardhi

Image
                   NA FATMA HAMAD, PEMBA WANAWAKE ambao ni wakulima wa kilimo msitu, shehia ya Mchanga mdogo wilaya ya Wete Pemba, wamesema wanakabiliwa na changamoto ya umiliki wa ardhi, jambo linalowalazimu kuzitumia za wenzao wao. Walisema hawana mashamba yao,  na badalayake hulima katika ardhi za waume zao, jambo linalowapa hofu juu   ya kuendeleza kilimo chao hicho ama kinyume chake. Wakizungumza na mwandishi wa habazri hizi kwa nyakati tofauti juu ya maendeleo ya kilimo chao, walisema hilo haliwapi uhakika wa kilimo hicho, kutokana na hofu ya kibinaadamu.   Walisema licha ya matamko mbalimbali za kisheria na   kidini, kuelezea haki zao juu ya umiliki wa ardhi, lakini bado jamii hawajalipa kipaumbele na kuendelea kutumia ardhi za watu wingine. Mmoja kati ya wakulima hao,   Fatma Hamad Bakar, alisema kwa mwaka wa pili sasa, anaendeshe kilimo hicho, katika shamba la aliyekuwa muume wake, ambae hadi s...

MGOMBEA URAIS ADC AAHIDI FUPA KWA WALIMU WA MADRASA AKIPATA URAIS

Image
                                 NA FATMA HAMAD,PEMBA MGOMBEA Urais Zanziba kwa tiketi ya Chama cha Allance for Democratic Change ADC Hamad Rashid Muhamed amesema endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi na kuwa Rais, atahakikisha walimu wa Madrasa za Qur an  wanalipwa mishaha kama walimu wengine. Mgombea huyo ameyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho, katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni uliofanyika Gombani ya kale Chakechake mkoa wa Kusini Pemba. Alisema walimu wa Madrasa sikuzote wamekua wakiishi katika maisha ya unyonge, hivyo endapo atachaguliwa atahakikisha walimu wote wa madrasa  wanapokea mishahara kila mwezi. ‘’Tunaona walimu ambavyo  wanapoteza muda wao madrasani kwa kutusomeshea watoto wetu elimu ya akhera, lakini tukiangalia maisha yao bado ni ya kusikitisha,’’alisema Alisema  kwa vile elimu wanayoifundisha ndio msingi wa mais...

WANAFUNZI DARASA LA SABA LEO KUANZA MITIHANI YAO

Image
                       FATMA HAMAD, PEMBA Jumla ya wanafunzi 18236,  wa darasa la Saba  waleo hii waanza mitihani yao ya Taifa kisiwani Pemba, ambapo  wanawake ni  9235 ikiwa wanaume ni 9001. Akitoa tarifa hiyo Afisa Mdhamini wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa mwandishi wa habari hizi huko Ofisini kwake Chakechake mkoa wa Kusini Pemba  Alisema maandilizi yote ya Mitihani yameshakamilika, hivyo jumla ya wanafunzi  18236 watafanya mitihani yao katika vituo 139 kwenye Skuli mbalimbali kisiwani humo. Alisema kwa mwaka huu kutakua na jumla ya walimu wakuu 189, huku walimu watakaosimamia mitihani ni 608, huku walinzi kutoka Jeshi la Polisi ni 278. Aidha Afisa huyo aliwataka walimu kuhakikisha wanasimamia mitihani hiyo kwa uwadili na uwaminifu wa hali ya juu, ili kuepusha udanganyifu na wanafunzi kufutiwa  kwa mitihani yao. ‘’Walimu simamieni kwa uadilifu, kama Wizara ya Elimu hatupendi mwisho w...

KISIWAPANZA WALILIA HUDUMA ZA MAMA NA MTOTO

Image
                       NA FATMA HAMAD, PEMBA WANANCHI WA Kisiwapanza wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba, wamelalamikia juu ya ukosefu wa huduma za uhakika kwa wajawazito   katika kituo chao cha afya,   jambo linalopelekea kuhatarisha maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua. Walieleza kuwa katika kituo chao huduma za mama na mtoto bado hazijakua rafiki kwao, kwani kituo   kizima kuna muhudumu mmoja tu ambae anazalisha, na huenda wakati wa mchana tu. Walisema endapo mzazi atapata tatizo wakati anapokwenda kujifungua kituoni hapo, ama atakapoumwa na uchungu wakati wa usiku hulazimika kuvuushwa baharini na kupelekwa Hospitali kuu ya Abdallah mzee Mkoani, ambapo wengi   hujifungulia ndani ya boti, hali inayopelekea kuhatarisha usalama wa mama na mtoto. ‘’Kituo kizima daktari anaezalisha ni mmoja ivo vifaa vyenyewe navyo havipo vya kutosha, na ikifika jioni anaondoka ikitokezea mjamzito akiumwa usi...