Wajasiriamali walia na uhaba wa malighafi za kusarifia bidhaa.
WANAWAKE
WAJAsiriamali kisiwani Pemba wamelalamikia juu ya kukosa sehemu maalumu ya
kununulia malighafi kwa ajili ya kutengenezea bidhaa kama vile, Crab pamoja na sabuni.
Wajasiriamali hao wametoa kauli hiyo wakati wakizungumza na
mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumaliza mafunzo maalumu ya utengenezaji
wa bidhaa za vyakula kama vile Makwaru na Achari, huko Ofisi za Jumuiya ya
Uhifadhi wa Misitu CFP, Minyenyeni Wete Kaskazini Pemba.
Maryam Mbarouk Khamis
mjasiriamali kutoka Kambini Mchangamdogo na Aisha Ali Hamad wa kiuyu minungwini
walisema wamekua wakipata mafunzo kadhaa, lakini wanashindwa kuzalisha kutokana na kukosa
mali ghafi kwa ajili ya kutengenezea bidhaa hizo.
‘’Tunataka vitu tutengeneze lakini sehemu ya kununua ivo
vifaa vya kutenezea bidhaa kama vile Ckirabu, shampuu, sabuni hapana, mpaka tuagizishie
nje ya Pemba, hilo sisi wajasiriamali wachanga linatukwaza,’’walisema.
Walisema kwa vile serikali
ya awamu ya nane imedhamiria kuwanyanyua wajasiriamali wadogo wadogo, ni vyema
kuboresha miundombinu ya upatikanaji wa mali ghafi kwa kuweka kituo maalumu,
ili wajasiriamali hao iwe rahisi kuzipata na wazalishe bidhaa kwa wingi na
zenye ubora.
Mapema Mkufunzi wa mafunzo hayo ambae pia ni
mjasiriamali Meiye Mbarouk Mussa alisema
suala la upatikanaji wa malighafi pamoja
na vifungashio bado ni tatizo, jambo linalopelekea kutokuendele kwa
wajasiriamali wadogo wadogo.
‘’Nikweli suala la upatikanaji vifaa kama vyakutengenezea
Ckrabu, havipatikani hadi uagizie, hali inayowafanya wajasiriamali wengi
watengeneze bidhaa kimazoea,’’alisema.
Aidha aliwasisitiza wajasiriamali hao kuhakikisha
wanavisajili vikundi vyao katika mamlaka husika, viweze kuwa rasmi na viweze
kutambulika kisheria.
Pia aliwataka
wazisajili bidhaa zao katika mamlaka za ZBS, ZFDA NA BRA, kutasaidia kua
zenye ubora na zenye viwango ziweze kuuzwa ndani ya nchi, na hata katika soko
la Dunia.
‘’Takribani wanawake 180 tumewapatia mafunzo ya ujasiriamali,watengeneze
bidhaa waondokane na changamoto ya umaskini,’’alisema.
Mafunzo hayo ya siku tatu yaliowakutanisha wajasiriamali wadogo wadogo pamoja na wakulima wa kilimo msitu kutoka shehia za Mchangamdogo, Kambini, Kiuyu minungwini na Chwale, yameandaliwa na Jumuiya ya uhifadhi wa misitu Pemba CFP, ambapo lengo hasa ni kuwafundisha kutengeneza bidhaa mbali mbali, ili wajiingizie kipato chao wenyewe.
Afisa Habari wa Uwakala wa Uwezeshaji Wananchi kiuchumi ZEEA
Pemba Abdi Juma Suleiman, alikiri kuepo kwa changamoto hiyo ya upatikanaji wa
malighafi pamoja na vifungashio kwa wajasiriamali wa Pemba.
Alisema kwa sasa wako kwenye mchakato wa kuweka sehemu
maalumu katika eneo la wajasiriamali Michakaini Chakechake, bidahaa na
vifungashio viweze kupatikana hapo, ili kuondosha changamoto hizo.
‘’Tunatarajia kuweka duka maalu litakalokua na vifaavyote
ambavyo wajasiriamali wanasafirisha kutoka nje ya Pemba viweze kupatikana
hapo,’’alisema.
Alisema pia kutakuepo na Mshine ambayo itatoa vifungashio
pamoja na Brendi za biashara zao.
Sera ya Zanzibar ya Wajasiriamali Wadogo na wa Kati ya mwaka 2006 lengo lake ni kukuza sekta ya wajasiriamali wadogo na wa kati, kuendeleza biashara ndogo ndogo na ujuzi wa kiufundi miongoni mwa Watendaji.
Comments
Post a Comment