WANAFUNZI DARASA LA SABA LEO KUANZA MITIHANI YAO
FATMA HAMAD, PEMBA
Jumla ya
wanafunzi 18236, wa darasa la Saba waleo hii waanza mitihani yao ya Taifa
kisiwani Pemba, ambapo wanawake ni 9235 ikiwa wanaume ni 9001.
Akitoa
tarifa hiyo Afisa Mdhamini wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali kwa mwandishi wa
habari hizi huko Ofisini kwake Chakechake mkoa wa Kusini Pemba
Alisema maandilizi yote ya Mitihani
yameshakamilika, hivyo jumla ya wanafunzi 18236 watafanya mitihani yao katika vituo 139
kwenye Skuli mbalimbali kisiwani humo.
Alisema
kwa mwaka huu kutakua na jumla ya walimu wakuu 189, huku walimu watakaosimamia
mitihani ni 608, huku walinzi kutoka Jeshi la Polisi ni 278.
Aidha
Afisa huyo aliwataka walimu kuhakikisha wanasimamia mitihani hiyo kwa uwadili
na uwaminifu wa hali ya juu, ili kuepusha udanganyifu na wanafunzi
kufutiwa kwa mitihani yao.
‘’Walimu
simamieni kwa uadilifu, kama Wizara ya Elimu hatupendi mwisho wa siku kusikia
kama kunawanafunzi wamefutiwa mitihani yao.’’alisema.
Alisema
ni vyema kwa vyombo vya ulinzi na usalama
kushirikiana na walimu katika kusimamia mitihani, ili kuna imefanyika
bila udanganyifu na kupatikana kwa
matokeo mazuri.
Aidha
Mdhamini huyo aliwataka walimu kuhakikisha wanafunga kambi zote za wanafunzi,
wapate kupumzika na kujianda vizuri kwenye mitihani yao.
Pia
aliwataka wazazi kuwa karibu zaidi na wato wao katika kipindi hiki cha na
kuapatia huduma muhimu, ikiwemo chakula, vifaa kwa ajili ya mitihani, ili
kufanya vyema kwenye Mitihani yao.
Aidha
alisema kwa upande wa darasa la tatu watahiniwa watakaofanya mitihani yao ya
kupima maarifa ni 18427.

Comments
Post a Comment