Naibu Chauma asema: ‘’Chagueni viongozi wenye imani na Nchi yao’’

 


NA FATMA HAMAD, PEMBA

Wananchi wametakiwa  kuwachagua  viongozi  ambao  wanauthubu na wenye uzalendo na nchi yao, wanaoweza kusimama na kutetea shida zinazowakwaza wananchi wao.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Ukombozi wa Umma Chauma Zanzibar, Mohamed Masoud Rashid  wakati akizungumza na wanachama na wananchi wa chama cha Chauma, katika uzinduzi wa kampeni za wagombea wa Ubunge, Uwakilishi na Udiwani huko Tumbe wilaya ya Micheweni kisiwani Pemba.

Alisema wakati umepita wa kuchagua viongozi kwa ajili ya chama ama kwa cheo chake, bali ni vyema kuhakikisha wanawachagua ambao wanauchungu na nchi yao na wanauwezo wa kutetea kero za wananchi, sambamba na kuwaletea mabadiliko.

‘’Nduguzangu wanatumbe badilikeni msichague viongozi ambao hawana maendeleo, isiwe wanaishia kupiga kofi tu kwenye meza,’’alisema.

Aidha alisema endapo chama chao kitaingia madarakani, jambo la kwanza watakalolifanya ni kushusha bei za vyakula, ili kuona kila mwananchi anakula mlo uliotimia.

‘’Bado wananchi wetu wanakabiliwa na tatizo la lishe duni, hivyo mkituchagua tutahakikisha kila mwananchi anapata chakula cha asubuhi, mchana, usiku na kilichokamilika,’’alieleza.

Mapema Mwenyekiti wa Vijana wa Chauma Zanzibar Fatma Omar Salim, aliwataka vijana kuwachagua viongozi wa Chama hicho, ili wawaletee mabadiliko.

Alisema vijana wengi wamekua wakizurura ovyo mitaani kutokana na kukosa ajira, hivyo endapo watakipigia  kura chama cha Chauma, kitaondosha ubaguzi na kuleta miradi ya maendeleo ambayo itatoa ajira, na vijana watajikomboa kiuchumi.

‘’Chama cha Chauma ndio mkombozi pekee kwa vijana, hivyo kichagueni ili mjemfaidi matunda yake,’’alieleza.

Fatma Yussuf Mohamed Katibu Mkuu Ngome ya wanawake Zanzibar alisema Sera za  Chama chao zimeonesha dhamira njema za kutaka kuwakomboa wananchi na janga la njaa, umasikini.

Alisema endapo wananchi watakiunga mkono kwa kukipa kura za ndio, suala la umasikini wa kipato kwa mtu mmoja mmoja litabakia historia.

Kwa upande wake Makamo Mwenyekiti wa Chama cha Chauma Zanzibar,  Issa Abass Hussein aliwanasihi wananchi kuhakikisha wanawachagua viongozi ambao ni wazawa, wanaozifahamu shida zilizomo kwenye majimbo yao, na sio kuwachagua kwa sababu ya kipato chao.

‘’Niwaombe ndugu zangu asije mtu akawadangaja kwa pesa ya maramoja, wachagueni nduguzenu wanazijua kero zenu, ili wapate kuzisemea na kutatuliwa,’’alisisitiza.

Aidha kwa upande mwengine aliwataka wananchi hao kuwapigia kura viongozi wanawake katika majimbo yao wawaletee mabadiliko, kwani wao ni wapenda maendeleo, Amani na ushirikiano na ni waaminifu.


Nao Vijana wa Tumbe waliahidi kukiunga  mkono chama hicho,ili kiltie mabadiliko kwao.

Walisema walishachokana na ahadi za uongo ambazo wamekua wakiwekewa na viongozi waliopita, hivyo watahakikisha wanakipa kura Chama hicho, kiweze kuwapatia mahitaji yao wanayoyahitaji ikiwemo ajira.

 


 

 

Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO