‘’KIMBILIENI HOSPITALI NA SIO KWA WAGANGA MNAPOONA DALILI ZA TB’’
WANANCHI wamehimizwa kujitokeza Hospitali kupima
afya zao wakati wanapojihisi na dalili za ugonwa wa Kifua kiku,ili waweze
kugundulika na kupatiwa tiba mapema, na sio kukimbilia kwa waganga wa jadi.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa
Habari Tehama na Mawasiliano kutoka Kitengo shirikishi Ukimwi, Homa ya Ini,
Kifua kikuu, na Ukoma Khalifan Khamis Khalifan wakati akizungumza na mwandishi
wa habari hizi huko Ofisini kwake Chak chake mkoa wa Kusini Pemba.
Alisema kwa mujibu wa utafiti
wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
unaonesha kwamba ugonjwa wa kifua kikuu upo, ingawa bado wagonjwa
kugundulika ni shida.
Alisema takribani asilimia 80 ya wagonjwa kuwagundua
inapotea, na hubakia katika jamii na
kutumia dawa za waganga wa jadi.
‘’Licha ya jitihada mbalimbali
zinazofanyika kuondosha ugonjwa huo, bado watu hawaji Hospitali, wanaendelea
kwenda kwa waganga wa jadi kwani wanaimani kwamba wamerogwa,’’alisema.
Alisema wananchi waliowengi
wanaamini kwamba Kifua kikuu ni maradhi yatokanayo na ushirikina, hivyo
hukimbilia kwa waganga jambo linalopelekea kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa
huo.
‘’Mtu anapoona dalili za kifua
kikuu haji Hospitali na hata anaekuja na tukamgudua hatumii dawa zetu bali
anatumia mitishamba, na kupelekea wengi kupoteza maisha,’’alieleza.
Alisema ugonjwa wa kifua kikuu
unatibika, hivyo ni vyema wanajamii kufika Vituo vya afya kupima afya zao
kuweza kugundulika na kupatiwa tiba mapema, ili kuepusha kuenea kwa mambukizi
ya maradhi hayo.
Alifahamisha kuwa ugnjwa wa
Kifua kikuu unaambukizwa kwa njia ya hewa, hivyo mgonjwa anaeugua maradhi hayo na kama
hajanza kutumia dawa inakua ni rahisi zaidi kuambukiza.
‘’Mtu ambae anaugua ugonjwa huo
kama hajaanza matibabu ni rahisi zaidi kuambukiza, hivyo anapokohoa anatakiwa
ajizibe mdomoni kwa mikono yake ama kwa kitambaa, ili kuwanusuru na
wengine,’’anaeleza.
Akitaja dalili za ugonjwa huo
ni kukohoa kwa muda wa wikimbili mfululizo au zaidi, kupungua uzito ama kukonda
bila sababu yoyote, kupata Homa mara
kwa mara hasa inapofika wakati wa jioni.
Aidha dalili nyengine ni
kutokwa na jasho jingi wakati wa usiku licha ya kua ni wakati wa baridi, pia
kukohoa makohozi ambayo huwa yamechanganyika na damu.
Alisema matibabu ya maradhi
hayo ni miezi sita mfululizo, ambapo dawa ni bure na zinapatikana masaa 24, bila ya gharama
yoyote.
Alisema maranyingi wagonjwa
wanaowapata na kuwaanzishia matibabu ni wale ambao walishashindikana kwa
waganga, na kuamua kuenda Hospitali.
Fatma Khamis Ali (sio jina lake
halisi) mkaazi wa kisiwa cha Pemba alisema baada ya kuumwa na kifua alikwenda
kwa mganga na kutumia dawa, ingawa hakupata nafuu hadi alipokuja Hospitali na
kuanza dawa za kufua kikuu alipata
ahueni.
‘’Nilishahangaika kwa muda wa miaka
miwili sijafanikiwa, ila nilipokuja Hospitali nikagundulika nina TB,
nilianzishiwa dawa na sasa nashukuru niko vizuri,’’alisema.
Mkurugenzi mkuu kutoka Shirika
la afya Duniani WHO Dokta Tedros
Adhanom Ghebreyesus alisema ingawa
juhudi za kimataifa za kutokomeza Kifua Kiku
zimeshaepusha vifo Milioni 750 tangu mwaka 2000, bado ugonjwa huo
unasababisha vifo vya watu Milioni 1.3 kila mwaka, na kuathiri mamilioni
wengine huku madhara yakisalia kwa Jamii na familia.
Dokta huyo alizungumza katika taarifa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la afya Duniani
huko Geneva, Machi 18 2024.
Pia kwa mujibu wa WHO mwaka
2022, iliripoti kukwamua vizuri katika kufanikisha upatikanaji wa huduma
ya uchunguzi, dhidi ya kifua kikuu na matibabu.


Comments
Post a Comment