Mgombea Urais ADC Aahidi kupunguza kodi wakati akiingia madarakani.

 


            NA FATMA HAMAD,PEMBA

MGOMBEA Urais Zanziba kwa tiketi ya Chama cha Allance for Democratic Change ADC Hamad Rashid Muhamed amesema endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi na kuwa Rais, atahakikisha anapunguza mtiririko wa kodi, ili kupunguza bei za bidhaa na kila mwananchi amudu kununua.

Mgombea huyo ameyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi pamoja na wafuasi wa chama hicho katika mkutano wa kampeni uliofanyika Micheweni Kaskazini Pemba.

Alisema  ushuru  wa bidha umekua mkubwa, na kupelekea bidhaa kupanda bei, hali inayowakosesha baadhi ya wananchi wenye kipato cha chini kushindwa kupata chakula cha uhakika.

‘’Nitakapo kua Rais nitahakikisha napunguza asilimia 10 ya kodi, na kila mfanyabiashara atakua na tin namba yake ya kulipa, ili kupunuza mtiririko na ubadhilifu,  na  mapato  yaingie serikali moja kwa moja,’’alieleza.

Aidha kwa upande mwengine Mgombea huyo alisema atahakikisha analiboresha Mwani kwa kuweka  Viwanda vya kisasa vya kuchakatia mwani, ili kuona makampuni ya nchi za nje yanafika Zanziba kununua zao hilo.

‘’Kisiwa cha Pemba tu kunazalishwa tani zaidi ya tani elfu 11 za mwani, hivyo ndani ya siku 100 tukiingia madarakani, tutaweka viwanda vya kisasa, na tutakua tunauza mwani, unga wa mwani pamoja na bidhaa zinazotokana na mwani alisema.

Alisema atalifanya zao la mwani linalozalishwa Zanzibar kua zao kuu la Taifa, na liweze kuuzwa Duniani kote, ili wakulima wafaidike na kilimo hicho.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama hicho Mwalim  Mohamed alisema endapo watachaguliwa na kuingia madarakani watatoa vifaa vya kisasa kama Maboti kwa ajili ya uvuvi, kwa wananchi wanafanya shughuli za uvuvi.

‘’Ndugu zangu wa Micheweni tunafahamu nyinyi uchumi wenu mmeuwelekeza zaidi baharini, hivyo endapo mtatuchagua, tutawapatia Boti za kisasa pamoja na elimu ya uvuvi wa kisasa, ili kupatikana kitoweyo cha kutosha.’’alisema.

Alisema ni vyema kwa mwaka huu wananchi wa Micheweni kura zao wakaziweka kwenye Chama hicho, ili kiweze kubadilisha maisha yao.

Mapema Mgombea Ubunge jimbo la Micheweni wa chama hicho Hamad Abdala Chande aliwataka wananchi wa Micheweni kuchagua viongozi ambao wanaumwa na wananchi na wenye sifa ya kua viongozi, na sio kuchagua kwa ajili ya chama Fulani.

Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo walisema ADC ni chama ambacho kimeonesha muelekeo mzuri, hivyo haja kwa jamii kukipigia kura cjhama hicho ili kuleta mabadiliko ya kimaendeleo.


Comments

Popular posts from this blog

KERO YA MAJI, TATIZO KWA WANAKIJIJI CHA GOMBEUME

HIVI NDIVYO UTELEKEZWAJI WA WATOTO UNAVYOATHIRI MALEZI, MAKUZI YAO

DNA YA THIBITISHA, MTUHUMIWA NDIE BABA MZAZA WA MTOTO