MGOMBEA URAIS ADC AAHIDI FUPA KWA WALIMU WA MADRASA AKIPATA URAIS
NA FATMA HAMAD,PEMBA
MGOMBEA
Urais Zanziba kwa tiketi ya Chama cha Allance for Democratic Change ADC Hamad
Rashid Muhamed amesema endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi na kuwa
Rais, atahakikisha walimu wa Madrasa za Qur an
wanalipwa mishaha kama walimu wengine.
Mgombea huyo ameyasema hayo wakati akiwahutubia wananchi
pamoja na wanachama wa chama hicho, katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni
uliofanyika Gombani ya kale Chakechake mkoa wa Kusini Pemba.
Alisema walimu wa Madrasa sikuzote wamekua wakiishi katika
maisha ya unyonge, hivyo endapo atachaguliwa atahakikisha walimu wote wa
madrasa wanapokea mishahara kila mwezi.
‘’Tunaona walimu ambavyo
wanapoteza muda wao madrasani kwa kutusomeshea watoto wetu elimu ya
akhera, lakini tukiangalia maisha yao bado ni ya kusikitisha,’’alisema
Alisema kwa vile
elimu wanayoifundisha ndio msingi wa maisha lakini hakuna yoyote anaewaangalia, hivyo endapo
atachaguliwa atahakikisha anawawekea mazingira rafiki, waendeleze kitabu
kitakatifu cha Alla ( S,W).
Aidha kwa upande mwengine mgombea huyo alivitaka vyama
vyengine vya siasa kuhakikisha wanafanya
kampeni za kistaarabu, ambazo hazitasababisha kutokea kwa uvunjifu wa Amani
Nchini.
Akitoa salamu kutoka kwa Jumuia ya akinamama mwenyekiti wa wanawake Taifa
Nadhira Ali Haji amemtaka Rais wa Jamuhuri ya Muungano Tanzania Samia Suluh
Hassan kuweka usimamizi wa hali ya juu
katika suala la uchaguzi, ili kunusuru maafa na kuona umemalizika katika hali
ya amani na utulivu.
‘’Jicho letu lote lipo kwako wewe mwanamke mwenzetu sisi ni
watu wa Amani hatutaki kudhulumiwa, hatutaki kunyanyaswa, tunakuomba usimame
imara, ili tubaki salama kabla na baada ya uchaguzi,’’alisema.
Aidha kwa upande mwengine liwataka watoto kujiepusha na makundi ya kisiasa, ili
kujinusuru na vitendo viovu vya uvunjifu wa amani.
Alisema watoto muda wao wa siasa haujafika bali waendelee na
masomo yao, ili kuleta matokeo mazuri kwenye mitihani yao.
Kwa upende wake Mwenyekiti wa chama cha ADC Shaaban Ramadhan
Itutu alisema Zanziba uchumi wake unategemea zaidi bahari, hivyo endapo
wataingia madarakani wataimarisha uchumi
wa buluu na viwanda.
Alisema Zanziba imejaaliwa na rasilimali nyingi, hivyo mara tu watakapoingia madarakani watapigania suala la uchimbaji wa mafuta kuona yanachimbwa
na kupatikana, ili kuondosha umasikini
kwa wanchi wa visiwa hivyo.
Nae Mgombea wa Urais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania
kupitia chama hicho Wilson Elias Malumbe
alisema mara baada ya kuingia madarakani atahakikisha kunapatikana kwa Katiba
mpya, ili kuondosha mpasuko na mvurugiko uliomo katika vyama vya siasa.
Comments
Post a Comment